Na
Lydia Churi, Mahakama, Songea
Mahakama Kuu, Kanda ya
Songea imefanikiwa kwa asilimia 100 kumaliza kesi zote zenye umri unaozidi
miaka miwili Mahakamani.
Akitoa taarifa ya hali
ya kesi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Songea, Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo Mhe.
David Mrango alisema hadi kufikia Desemba 2016, Kanda yake ilikuwa na kesi 28
za jinai.
Alifafanua kuwa kesi za
jinai zilizofunguliwa kati ya Januari na Mei mwaka huu zilikuwa 51na
zilizomalizika na kutolewa hukumu ni 52 na zilizobaki kesi 27.
Kwa upande wa kesi za
madai , Jaji Mrango alisema mpaka Desemba 2016, kulikuuwa na kesi 46 za madai
kwenye Kanda yake , jumla ya kesi za madai zilizofunguliwa kati ya Januari na
Mei 2017ni 42 na zilizosikilizwa na kutolewa hukumu ni 47 wakati zilizobaki ni
kesi 41.
Alisema kati ya Januari
na Mei, vikao viwili vya kesi za mauaji vilifanyika ambapo kesi 22
zilisikilizwa na 18 zilitolewa hukumu huku 2 zikibaki.
Kuhusu upatikana wa
nakala za hukumu, Jaji Mfawidhi huyo alisema licha ya changamoto zilizopo,
Kanda yake imekuwa ikitoa nakala za hukumu pamoja na mienendo ya kesi kwa
wakati.
Mahakama kuu, Kanda ya
Songea ni moja ya Kanda za Mahakama Kuu 13 nchini, Kanda hii ina jumla ya
Majaji wawili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni