|
Jaji
Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Beatrice Mutungi akifungua kikao cha
Mahakimu wa Kanda ya Dar es salaam kilichohusu umuhimu wa maadili ya uhakimu na
utumishi wa umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya
Bunge uliopo jijini
Dar
es Salaam.
|
|
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya
Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akizungumza na baadhi ya Mahakimu
mbalimbali wa Kanda ya Dares Salaam
kuhusu umuhimu wa maadili na Utumishi wa Umma katika kikao kilichofanyika
mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya Bunge uliopo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Kamishna wa kutoka Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe.
Jaji Amon Nsekela na kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam Mhe.
Beatrice Mutungi.
|
|
Kamishna
kutoka Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Jaji Amon Nsekela
akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa maadili ya Uhakimu na Utumishi wa Umma
kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi mdogo wa Bunge uliopo jijini
Dar es Salaam.
|
|
Baadhi wa mahakimu wa Kanda ya Dar
es Salaam wakiwa katika kikao kilichohusu umuhimu wa maadili na
Utumishi wa Umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa ofisi ndogo
ya Bunge uliopo jijini Dar es Salaam. Kanda ya Dar es salaam inahusisha mikoa
ya Morogoro na Pwani.
|
|
Baadhi ya viongozi wa meza kuu
wakifuatilia mada ya Msajili ya Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Ilvin Mugeta
(hayupo pichani) wakati wa kikao kilichohusu umuhimu wa maadili na
Utumishi wa Umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa ofisi ndogo
ya Bunge uliopo jijini Dar es Salaam.
|
|
Msajili
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta, akitoa mada kuhusu maadili ya
kazi ya Uhakimu wakati wa kikao kilichohusu umuhimu wa maadili na
Utumishi wa Umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi mdogo
wa Bunge uliopo jijini Dar es Salaam.
|
Na Magreth Kinabo
Jaji Kiongozi wa
Mahakama ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali, amewataka Majaji na Mahakimu
kuzingatia maadili ya Uhakimu na
Utumishi wa Umma na kutenda haki kwa wakati wanapotimiza majukumu yao.
Aidha, Jaji huyo alisema
Majaji na mahakimu wanaptimiza majukumu yao wanapaswa kuzingatia kanuni za
utendaji wao na za utumishi wa umma hatua ambayo itawafanya kukidhi matakwa ya
wananchi wanaowahudumia.
Kauli hiyo, imetolewa na
Mhe. Jaji huyo wakati akizungumza na
baadhi ya Majaji na Mahakimu mbalimbali
katika kikao kilichofanyika mwishoni mwa
wiki kwenye ukumbi mndogo wa Bunge uliopo jijini Dar es Salaam.
“Suala la maadili
lilianza tangu enzi za kale, jamii ilikuwa inajiwekea maadili, uwepo wa maadili
ni heshima na utii, tabia ya uaminifu, uwajibikaji na kufuata utaratibu kila unapotekeleza kazi,”
alisisitiza Mhe. Jaji Kiongozi huku akisema masuala yalizishazungumziwa na
baadhi ya viongozi wa kitaifa, akiwemo Baba wa Taifa mwaka Machi 15, mwaka 1984 na Rais Mstaafu Benjamin
Mkapa Novemba 27, mwaka 2011.
Aliongeza kuwa suala la
maadili ni muhimu katika kupambana na rushwa, pia linafanya Jaji na Hakimu awe
na tabia njema mbele ya jamii, hivyo kazi hizo zinahitaji uadilifu na mtu mwenye
hofu ya Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake Jaji
Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Beatrice Mutungi akifungua kikao hicho,
alisema kuwa lengo la kikao hicho lilikuwa kujadili changamoto za kada hizo na
kubadilishana uzoefu wakati wa kutatua changamoto hizo.
Kikao hicho kilihudhuriwa
na baadhi ya viongozi mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni