Pichani ni Mtendaji,
Mahakama ya Hakimu Mkazi-Njombe, Bi. Maria Francis Itala, Bi. Itala alisema
kuwa Mahakama mkoani Njombe wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa
Watumishi wa Kada mbalimbali. Alisema kwa sasa Mkoa huo una jumla ya Watumishi
78 na uhitaji wa Watumishi ili kutekeleza Majukumu tofauti tofauti ni 359,
hivyo kuna upungufu wa Watumishi 281.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Makambako lililopo mkoani Njombe, hali ya miundombinu ya Majengo katika mkoa huu inaridhisha kwa wastani ingawa kuna baadhi ya maeneo ambayo majengo yake yanahitaji kufanyiwa ukarabati au kujengwa kutokana na kutokuwepo kwa majengo kabisa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya Godfrey (kushoto) akiwa katika ukaguzi
maalum alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Kalenga-Iringa ili kujionea hali ya utendaji
kazi katika Mahakama hiyo.
Moja ya vitu
alivyokagua Hakimu huyo Mfawidhi, Mhe. Kalenga ni pamoja na Rejesta ya Mahakama
ya Mwanzo Kalenga kuangalia kama rekodi zinajazwa vizuri kulingana na aina ya
kesi zinazofunguliwa.
Pichani ni muonekano wa
jengo la Mahakama ya Mwanzo Kalenga- Iringa ambapo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya-Iringa amefanya ukaguzi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya alipomaliza kusaini kitabu cha wageni
pindi alipowasili katika Mahakama ya Mwanzo Kalenga kwa ajili ya ukaguzi wa
Mahakama hiyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya Godfrey akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Kalenga mara baada ya kukamilisha shughuli ya ukaguzi iliyompeleka katika Mahakama hiyo. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni