Kwa miaka ya hivi
karibuni Mkoa wa Mtawara umekuwa na maendeleo makubwa ya Kichumi na ya Kisiasa.
Kutokana na mabadiliko hayo maendeleo ya Mkoa wa Mtwara yameongeza ari na
matumaini mapya ya maisha bora kwa wananchi wa Mkoa huo.
Mtwara ya sasa ni yenye
fursa lukuki kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo yaliyotokana na
uchimbaji wa gesi asilia, maendeleo ya
uboreshaji wa miundombinu na ongezeko na mapato katika zao la korosho.
Maendeleo haya yameikumba Sekta mbalimbali Mkoani
humo ikiwemo ya Sekta ya Sheria hususani Mahakama. Mahakama ya Tanzania kanda ya Mtawara yenye watumishi 218
ilianza kutekeleza Mradi wa Mapambano dhidi Rushwa (Strengthening
Tanzania Anti-Corruption Action ) kwa kifupi STACA Mwaka 2011/2012 chini ya
ufadhili wa Uingereza kupitia Shirika lake la misaada la Kimataifa la DFID.
Lengo kuu la mradi huu
ilikuwa ni kuzuia na kupambana na rushwa mahala pa kazi, Katika Mkoa wa Mtwara
mradi huu ulihusisha Wilaya zote tano za
Tandahimba, Masasi, Newala, Mtwara na Nanyumbu. Mradi huu ulijikita katika
ugawaji wa vitendea kazi kama kompyuta na ‘printer’ zake, mafaili ya kufungulia mashauri (case
files), makabati ya kutunzia mafaili na kumbukumbu, pikipiki kwa watumishi wa Mahakama pamoja na
baiskeli kwa ajili ya kusambazia ‘Summons.’
Hata hivyo, Mradi pia
ulichapisha na kugawa vibonzo mbalimbali vyenye matangazo dhidi ya vitendo vya rushwa Mahakamani
na ugawaji wa simu za mkononi kwa ajili ya kupokea malalamiko kwa wakuu wa Wilaya,
Mikoa, Mahakama pamoja na wadau.
“Tulifanya tathmini kimkoa na kuzumgumza na
wahusika wenyewe yaani watumishi, imeonekana tumefanya vizuri sana’’ alisema
Mtendaji wa Mahakama Mkoani Mtwara Bw. Selestine Onditi.
Alieleza kuwa, kwa
ripoti waliyonayo kwa upande wa rushwa hakuna malalamiko yaliyopokelewa
yaliyohusu rushwa moja kwa moja. “Kwa maana hiyo, mradi wa STACA umefanya kazi kubwa”
alisisitiza Mtendaji huyo wa Mahakama Mkoani Mtwara.
Tathmini ya taarifa ya simu za mkononi zilizogawiwa kwa Watendaji
mbalimbali Mkoani Mtwara na Mahakama kwa
ujumla inaeleza kuwa hakuna lalamiko lolote lililohusu rushwa bali kulikuwa na
malalamiko mengine kama ya ucheleweshwaji wa mashauri pamoja na nakala za
hukumu.
Alieleza kuwa, mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia mradi huu ni
pamoja na mahakama za mwanzo kuwa ndio waliofaidika kwa kiasi kikubwa kutokana
na mradi huu, kasi ya usikilizwaji wa mashauri katika Mahakama za Mwanzo
uliongezeka kwa 90%, kasi ya utoaji wa nakala ya hukumu imeongezeka sana karibu
96%, huku hatuchelewi hukumu zinatolewa kwa
muda ’’ alisisitiza Mtendaji huyo.
Makabati ya kutunzia
mafaili ya kesi (case files) imesaidia katika utunzaji wa kumbukumbu, kabla ya
hapo ilikuwa kupata faili lazima ukutane na mafaili yenye vumbi ndio lianze kushughulikiwa
hii ilisababisha kuleta viashiria vya Rushwa kwa wateja waliokuwa wanapata
huduma katika Mahakama zetu. Hali ilikuwa mbaya sana Mahakama nyingi hasa za mwanzo
ndizo zilikuwa na matatizo ya utunzaji wa kumbukumbu.
Mafanikio mengine ya
mradi huu ni pamoja na kuongeza ari na mazingira bora ya kufanyia kazi kwa
watumishi wa mahakama. Baadhi ya watumishi wa Mahakama kupewa vifaa vya
maofisini ,baiskeli na pikipiki. Hii imeongeza ari ya kufanya kazi zaidi kwa
watumishi wa Mahakama.
Baadhi ya pikipiki zilizotolewa chini ya Mradi wa STACA, pikipiki hizi na baadhi ya vifaa vingine tajwa ni miongoni mwa vitendea kazi vilivyotolewa kurahisisha utoaji huduma ya haki.
Baiskeli zinatumiwa
kusambaza barua za wito wa kuhudhuria Mahakama (Summons), pikipiki zina tumiwa
na Mahakamimu kwenda na kurudi kazini pamoja na kuhudhuria vikao vya na Mahakama zinazotembelewa. Hii imeleta ujasiri
wa kazi,kujituma kwa watumiishi lakini kikubwa zaidi imeleta utandawazi (transparency)
katika shughuli za Mahakama ambapo kwa
sasa shughulizo zote za Mahakama hakuna siri tena.
Mabango ya matangazo ya
mapambano dhidi ya rushwa yamebandikwa
katika ofisi mbalimbali za Serikali ikiwemo ofisi wa Mkuu wa Mkoa,Wakuu wa Wilaya,
TAKUKURU ,Mahakama, pamoja na sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi. Kimsingi,
sasa wananchi walio wengi wanaimini Mahakama kama mkombozi wa haki zao na ndio
tegemeo pekee la kukimbilia wakiwa na shida.
Kwa mantiki hiyo, hali
ya wananchi kuikubali Mahakama imeongezeka
kufikia 80% ukilinganisha 50% ilivyokuwa huku nyuma. “Haya ni mafanikio makubwa
ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya Mkoa wa Mtwara’’ Alieleza Bw.
Onditi. Kwa mafanikio haya ya mradi wa STACA yametokana kwa pamoja na
kutekeleza Mpango
Mkakati Mahakama wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania
baada ya kufanya mafunzo katika ngazi mabalimbali katika mkoa wa Mtwara.
Mafunzo yalisaidia kwa kila mtumishi wa Mahakama kutekeleza majukumu yake. Kwa
shapa mtawara kila tunapokuwa na mikutano au mafunzo yoyote huwa taunaanza na
dozi ya Mpango Mkakati kwanza. ‘’ Hii ndio siri ya mafanikio katika kutekeleza
shughuli za Mahakama Mkoani Mtwara.
Muonekano wa picha ya
bango lenye ujumbe wa kuzuia na kupambana na Vitendo vya Rushwa ikiwa
imebandikwa katika jengo la Mahakama Kuu-Kanda ya Mtwara. Bango hili ni kati ya
Mabango mengi ambayo yamebandikwa katika majengo ya Mahakama nchini lengo
likiwa ni kuzuia rushwa na vitendo vitendo vyenye ukosefu wa maadili.
Hata hivyo, pamoja na
mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Mradi wa kupambana na Rushwa Mkoani
Mtwara pamoja na kutekeleza Mpango Mkakati wa Mahakama wa miaka mitano kuna
baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mradi STACA kwa
baadhi wa wadau kuomba mradi huu kuwa endelevu kwani kwa sasa mradi umemaliza
muda wake, Mabango yamesaidia sana kupunguza masuala ya Rushwa, kwa tathmini ya
Mkoa walipata mabango karibu 200 lakini hayakutosha kusambazwa katika taasisi
zote Mkoani humo wakiwamo wadau wa Mahakama.
Kuhusu matumizi ya simu kwa ajili
ya kutuma taarifa (sms) kwa watumiaji wa kawaida, changamoto kubwa ilijitokeza
ni kwa watu wengi kutopenda kutuma ujumbe mfupi na wengi wapependa simu
zitumike kwa kupiga na kuzungumza moja kwa moja.Sababu nyingine ni kwa baadhi
ya wananchi kutojua kusoma na kuandika, hivyo kutoweza kutumia namba za
malalamiko kwa ajili ya kutuma malalamiko yao.
Changamoto nyingine ya
ujumla kwa mkoa wa Mtwara ni uchakavu wa majengo hasa katika Mahakama za Mwanzo
na hataka hata jengo la Mahakama Kuu kanda ya Mtwara ndio liko katika hatua ya
mwisho ya kumalizia ukarabati.Hata hivyo hatua za awali kwa ajili ya kujenga
jengo jipya la Mahakama Kuu kanda ya Mtwara inaendelea.
Ni mategemeo ya
watumishi wa Mahakama pamoja na wadau
kuwa, Mahakama Tanzania itendeleza
mradi wa STACA Chini ya ufadhili wa shirika la DFID la Uingereza ili uendane sambamba na utekelezaji wa Mpango
Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama unaotekelezwa kwa pamoja na Washirika wa
maendeleo kama Benki ya Dunia.Pamoja na mambo hayo yote Mahakama ya kanda ya
Mtwara inaendelea vizuri na kazi yake ya kutoa haki kwa wakati na kujenga imani
imara kwa wananchi, kama chombo muhimu cha utoaji haki Mkoani humo.
Kwa upande wake,
Mratibu wa Mradi wa STACA-Mahakama ya Tanzania, Bi. Wanyenda Kutta anasema
Mradi huo umefanikiwa kwa asilimia 100 akieleza kuwa kazi ambazo zilipangwa
kutekelezwa chini ya mradi zilitekelezeka kwa asilimia 100 na kama kuna
mapungufu ni kutokana na Jiografia ya Mkoa mmoja hadi mwingine.
Hongera Mahakama kwa kazi nzuri mnazofanya. Juhudi zenu zinaonekana mmekuwa tofauti na zamani. Mfike na Musoma pia tupate Mahakama tusiende Mwanza. Musoma pia tuletewe Jaji
JibuFuta