Jumamosi, 8 Julai 2017

JAJI MKUU WA ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA MAHAKAMA YA TANZANIA

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akipewa Maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga alipotembelea banda hilo leo.
 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akipewa Maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga alipotembelea banda hilo sehemu ya Mahakama Kuu.
 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza jambo na watumishi wa Mahakama alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzanaia sehemu ya Mahakama Kuu Divisheni ya kazi leo jijini Dar es salaam.

Afisa Ugavi wa kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama (JDU) Damasia Ndunguru akimuelezea Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu kuhusu Maboresho ya Mahakama ya Tanzania alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akiangalia ukuta uliojegwa kwa kutumia Teknolojia ya Moladi alipotembelea banda la wadau wa Mahakama (Moladi Tanzania). Mahakama ya  ya Tanzania inatumia Teknolojia ya Moladi kujenga baadhi ya Mahakama zake.
 Fundi Mchundo wa Mahakama ya Tanzania, Hassan Dunia akimuelezea Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu kuhusu ujenzi wa majengo ya Mahakama kwa kutumia teknolojia ya Moladi leo alipotembelea banda la wadau wa Mahakama (Moladi Tanzania).
 Fundi Msanifu wa Majengo wa Moladi Tanzania, Queen Mduma  akimuelezea Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu kuhusu teknolojia ya Moladi alipotembelea banda la wadau wa Mahakama (Moladi Tanzania).
  Katibu Mahususi wa Mahakama ya Rafani, Rukia Salim akimuelezea Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu jinsi Kurugenzi ya Malalamiko na Maadili ya Mahakama ya Tanzania inavyowahudumia wananchi.




Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga akimsindikiza Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu baada ya kumaliza kutembelea banda la Mahakama ya Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni