Waziri
wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi (pichani) akiongea na Watendaji
wa Mahakama pindi alipotembelea Mahakama ya Rufani (T) mapema leo na kuonana na
Kaimu Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama,Prof. Kabudi amehaidi kutoa
ushirikiano wa dhati kwa Mahakama katika utekelezaji wake wa jukumu la utoaji
haki nchini, katikati ni Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma,
kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.
Viongozi na Watendaji mbalimbali wa
Mahakama ya Tanzania na Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi pindi alipokuwa akitoa hotuba
yake pindi alipotembelea Mahakama ya Rufani mapema Julai, 14, 2017, Mhe. Kabudi
amempongeza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo, hii
ni mara ya kwanza Waziri kutembelea Mahakama tangu kuteuliwa kwake kushika
nafasi ya Uwaziri, Machi 24, 2017.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Prof. Ibrahim Juma (katikati) akiongea na Watendaji wa Mahakama na Wizara (hawapo pichani) pindi Waziri
alipotembelea Mahakama, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, wa kwanza kulia ni Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.
Kaimu
Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (kulia) akimkabidhi
vitabu vya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pindi
alipotembelea Mahakama ya Rufani mapema leo.
Mtendaji
Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kataanga akitoa taarifa juu ya
Utendaji kazi wa Mahakama mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria pindi Waziri
alipotembelea Mahakama, katika taarifa yake kwa Waziri, Mtendaji Mkuu
amesisitiza mabadiliko ya Kiutendaji ndani ya Mahakama, kupitia Mpango Mkakati
wake wa miaka mitano (5).
Mtendaji
Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akiendelea kutoa mada kupitia 'Projector.'
Jaji
Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno la
shukrani kwa Waziri wa Katiba na Sheria, mara baada ya majadiliano kukamilika.
Kaimu
Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Viongozi na Watendaji wa Mahakama na Wizara mara
baada ya kukamilika kwa majadiliano na Waziri wa Katiba na Sheria alipotembelea
Mahakama mapema leo, wa tatu kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof.
Palamagamba Kabudi, wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe.
Sauda Mjasiri, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Mussa
Kipenka, wa tatu kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.
Ferdinand Wambali, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria,
Mhe. Prof. Sifuni Mchome na wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara wa
Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju.
(Picha na MARY GWERA)
(Picha na MARY GWERA)
Na
Lydia Churi-Mahakama
Mahakama
ya Tanzania inayo nafasi kubwa katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha
inamaliza kwa wakati kesi hasa zile zinazohusu masuala ya kodi ili kuharakisha
maendeleo ya nchi.
Akizungumza
leo alipotembelea Mahakama ya Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi ameitaka Mahakama kuimarisha uadilifu na uwajibikaji ili
wananchi wapate haki zao kwa wakati.
Aidha,
Prof. Kabudi alisema anatambua na kuipongeza Mahakama kwa kupanga mikakati ya kuziondosha mahakamani kesi zote
za muda mrefu pamoja na kusogeza huduma kwa wananchi kwa kujenga na kukarabati
baaadhi ya majengo Mahakama.
Akizungumzia
suala la rushwa ndani ya Mahakama, Prof. Kabudi amewataka viongozi wa mahakama
kushughulikia suala hilo bila uwoga wala upendeleo.
Wakati
huo huo, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma amesema Mahakama
itaendelea kushirikiana kwa karibu na mihimili mingine ya nchi ili kuharakisha
maendeleo ya nchi.
Akizungumzia
kuhusu sheria, Prof. Juma alisema falsafa ya ni kwa namna gani sheria
zinufaishe uchumi wa watanzania ni muhimu kwa kuwa sheria zina mchango katika
wa uchumi wa nchi na zinasaidia katika kuondoa umaskini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni