Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa jana
alitembelea jengo la Mahakama Kuu Kanda
ya Shinyanga na kuipongeza Mahakama ya
Tanzania kwa jitihada zake za kuboresha
miundombinu ya Mahakama ili kuifanya iwe
ya kisasa. Waziri Mbarawa amepata pia nafasi ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Mhe. Jaji Mfawidhi-Shinyanga inayosimamiwa na TBA na amewaagiza TBA kusimamia kwa karibu ujenzi huo ili kuwaondolea adha ya kupanga kwa watu binafsi ambao wamekuwa na gharama kubwa za pango.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame akipatiwa maelezo kuhusiana na jengo la Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga na Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo Mhe. Richard Kibela pindi Waziri huyo alipotembelea jengo hilo.
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga Mhe. Richard Kibela (aliyeketi mbele) akimpatia maelezo juu ya Mahakama hiyo,Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa pindi alipotembelea Mahakama hiyo.
Jaji Mfawidhi pamoja na Waziri wakiendelea na majadiliano.
Mtendaji wa Mahakama, Kanda ya Shinyanga, Bw. Masanja akitoa maelezo khs Mahakama ya Shinyanga mbele ya Mhe. Waziri ambaye hayupo pichani pindi alipotembelea katika Mahakama hiyo, Julai 16, mwaka huu.
Muonekano wa ndani wa sehemu ya jengo la kisasa la Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga.
|
Jaji Mfawidhi wa Shinyanga yeye anaitwa nani? Hii inatia moyo kuona Waziri wa Ujenzi akiitembelea Mahakama kuona maendeleo ya Mahakama. Hatuna kumbukumbuka sisi wananchi kuona Mahakama inatembelewa na Waziri asiye wa Wizara ya Sheria na Mambo ya katiba. Pongeze kwa Waziri Mbarawa
JibuFutaYohana Wilbert
Futa