Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Upendo H. Msuya amefariki dunia usiku
wa kuamkia leo tarehe 19/7/2017 katika hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa
kuanzia Jana tarehe 18/7/2017.
Taarifa
iliyotolewa na Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe, Ferdinand Wambali
inasema Mahakama imepokea taarifa hizo za kusikitisha kutoka kwa familia ya
Marehemu.
Msiba
uko nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es salaam. Aidha, taratibu za
mazishi zinafanywa na taarifa itatolewa hapo baadaye.
Marehemu
Jaji Mstaafu Msuya alizaliwa tarehe 9 Desemba, 1957 katika wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Aliajiriwa na
Mahakama ya Tanzania kama Hakimu tarehe 1 Januari, 1983.
Aidha,
mwezi Oktoba mwaka 2007, Marehemu Msuya aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tume ya Haki
za Binadamu.
Aliteuliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
tarehe 24 Mei, 2008.
Baada ya kuugua kwa muda mrefu, Marehemu aliomba kustaafu
kazi ambapo Mhe. Rais aliridhia uamuzi huo Mei 15, 2017.
Mungu
ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni