Jumatano, 5 Julai 2017

KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA ATEMBELEA MAONESHO YA 41 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitembelea   Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu   Julius  K.Nyerere(Sabasaba)  vilivyoko  jijini Dar es salaam, Barabara ya Kilwa. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutageruka.
  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Willy Machumu  alipotembelea banda la Mahakama sehemu ya Mahakama ya Rufani kwenye  Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu  Julius  K. Nyerere(Sabasaba)  jijini Dar es salaam.
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni katika katika banda la Mahakama sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Aliyesimama mwenye miwani ni Jaji wa Mahakama Kuu 
Mhe. Edson  Mkasimongwa.





Anaeleza  ni  mwenye miwani ni Jaji wa Mahakama Kuu 

Mhe. Edson  Mkasimongwa kwa mwandishi wa habari.

 11
 Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania, Machumu Essaba akimuelezea Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma namna Mfumo wa  Kielektroniki wa Kusajili na Kuratibu Mashauri (JSDS) 
unavyofanya kazi. 
 Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga  akimuelezea jambo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kuhusu Mahakama ya Ardhi.
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini mara baada ya kumaliza kulitembelea banda la Mahakama ya Tanzania.

 Watumishi wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma mara baada ya kumaliza kutembelea mabanda  mbalimbali.

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akipata maelezo juu ya utengenezaji wa Samani za nyumbani katika banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).   
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akipata maelezo juu ya vifaa vya usalama katika maeneo mbalimbali ikiwemo majumbani alipotembelea banda la Maonesho la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).   
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitazama kwenye kifaa maalum kwa ajili ya shughuli za utafutaji wa mafuta alipotembelea banda la Maonesho la Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) jana jijini 
Dar es salaam.  


 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutageruka jana katika viwanja vya Sabasaba kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa. 


 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi alipotembelea Banda la Mahakama jana. Kulia kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mhe. Aisha Nyerere.  
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akisalimiana na watumishi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) alipowatembelea jana. 
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akisoma kipeperushi kwenye banda la Mahakama- TAWJA alipowatembelea jana. 
 
 Kaimu   Jaji  Mkuu  wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim  Hamis  Juma, amesema kwamba  Mahakama  ya Tanzania imejipanga  kusikiliza  kesi zilizokwama  zinazohusu   benki  kwamba ili ziweze kwenda kwa haraka  na  kulingana  na sera ya nchi, ikiwemo  kuwezesha  ukuzaji wa uchumi.

Kauli  hiyo ilitolewa  na jana Kaimu Jaji Mkuu huyo , wakati  alipotembelea  Maonesho ya  41 ya Biashara  ya Kimataifa ya  sabasaba  yanayoendelea  katika 
Viwanja  vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko, Barabara ya Kilwa Road jijini Dar es Salaam, ambapo  alizungumzia kuhusu mlundikano  wa kesi mahakamani  alisema Mahakama ya Tanzania  inafanya mikakati ya kuweza kuzipunguza.

“Tunahitaji  majaji zaidi ya 30 ili kuweza kupunguza mlundikano uliopo wa kesi zilizopo Mahakamani,” alisema Profesa .
Profesa  Juma  alisema  hayo, baada ya kutembelea  mabanda  mbalimbali  ya maonesho, ambapo  alisema  Mahakama ya Tanzania,  imepiga hatua  katika mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), akitolea  mfano 

Mahakama Kuu  ya Tanzania  Divisheni  ya Biashara, ambapo alishauri kwamba  mahakama zingine za chini ziweze kujifunza.
Profesa Juma  pia  alitoa ushauri kwa  watu wenye viwanda  nchini  kufuata  sheria  na taratibu, waweze kusajiliwa  kwa kuwa kufanya hivyo kutawafanya  washiriki kuongeza pato la Taifa na kukuza uchumi wa nchi.
 
“ Nimetembelea  Banda la Mkemia  Mkuu wa Serikali  nimeona  mazao na bidhaa mbalimbali,hivyo  ni vema  watu wanaotengeneza bidhaa wakasajiliwa  ili waweze kufuata  sheria  na taratibu  za nchi, kwa kuwa kufanya hivyo kutawezesha bidhaa zao kuwa bora  na  wataweza kuiwezesha nchi kuendelea kushiriki katika  uchumi wa kisasa,” alisema Profesa  Juma.

Katika  maonesho   hayo, Kaimu Jaji Mkuu huyo,  miongoni  mwa  mabanda  aliyoyatembelea  banda  la Mahakama  ya Tanzania, Jeshi  la Magereza , Banda la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam(UDSM),banda la  Wakala  wa  Mkemia  Mkuu wa Serikal(GCLA)i, banda la Mamlaka ya Vitambulisho  vya Taifa(NIDA).

Lingine ni banda la Wakala wa Usajili , Ufilisi  na Udhamini (RITA) Mamlaka ya Reli  Tanzania, na Mabanda la Mamlaka ya Reli Tanzania, Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC), Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC .

Muonekano wa  Banda la Mahakama ya Tanzania.
 
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni