Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Mahakama ya Pili ya Watoto nchini Tanzania baada ya ile iliyoko Kisutu Jijini Dar es salaam. Mahakama hii imejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF).
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akifungua Pazia kuashiria uzinduzi wa Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Katikati ni Mwakilishi wa UNICEF nchini, Stephanie Shanler na kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza wakati
wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.
Mwakilishi
wa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa
Mahakama hiyo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya Mhe. Noel Chocha akielezea historia ya Ujenzi wa Mahakama hiyo.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiwa kwenye hafla ya Hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya Watoto leo jijini Mbeya. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali na kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya Mhe. Noel Chocha .
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania
Mhe. Katarina Revokati (kushoto) akiwa na Jaji wa mahakama Kuu Mbeya, Mhe.Dkt. Mary Levira (katikati) na Mwakilishi wa UNICEF nchini Stephanie Shanler
wakati wa Uzinduzi huo.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali na kulia akielezea
jambo wakati viongozi hao walipoingia ndani ya jengoi lililozinduliwa.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mahakama pamoja na Mwakilishi wa UNICEF nchini mara baada ya kuzindua Mahakama ya Watoto.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu wa Mahakama zilizoko kanda ya Mbeya mara baada ya kuzindua Mahakama ya Watoto.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili wa Serikali wa kanda ya Mbeya mara baada ya kuzindua Mahakama ya Watoto.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mahakama ya Tanzania mara baada ya kuzindua Mahakama ya Watoto. Wa kwanza kulia waliosimama ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga.
Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakicheza Mziki wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya Watoto. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama ya Tanzania Bibi Wanyenda Kutta.
Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakicheza Mziki wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya Watoto.
Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakicheza Mziki wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya Watoto. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama ya Tanzania Bibi Wanyenda Kutta.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa kwenye Hafla ya Uzinduzi huo.
Baadhi ya wa Mahakama ya Tanzania wakiwa kwenye Hafla ya Uzinduzi huo leo jijini Mbeya.
MAHAKAMA YA PILI YA WATOTO NCHINI YAZINDULIWA MBEYA
Na Lydia Churi-Mahakama, Mbeya
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma leo amezindua rasmi Mahakama ya watoto katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo nchini kufikia mbili. Mahakama ya kwanza ya watoto iko Kisutu jijini Dar es salaam.
Mahakama hii ya Watoto iliyoanza kufanya kazi rasmi Aprili 18 mwaka huu jijini Mbeya pamoja na ile ya Kisutu zina kazi kubwa ya kuamua kesi za watoto wanaojikuta wana ukinzani na Sheria zinazohusu watoto nchini pamoja na kutafsiri sheria hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania alisema maendeleo endelevu ya Tanzania yatajengwa kwa misingi ya haki za watoto huku akinukuu andiko la shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na watoto (UNICEF) lisemalo maendeleo ya taifa lolote yatakamilika baada ya watoto kuwa na afya njema, salama pamoja na kupata elimu.
Alisema uzinduzi wa jengo la Mahakama hiyo ya watoto unaashiria safari ndefu iliyonayo Tanzania ya kuhakikisha haki za watoto zinalindwa kwa kuwa pia bado kuna mikoa mingi ambayo inahitaji huduma hii muhimu.
Prof. Juma alisema kazi kubwa ya Mahakama ya Tanzania ni kutoa tafsiri pana ya sheria zinazohusu haki za watoto ili kupanua wigo wa ulinzi kwa watoto huku akiwataka Majaji na Mahakimu nchini kutafsiri sheria hizo ili zitekeleze wajibu wao kisheria.
Akitolea mfano wa Sheria ya Watoto namba 21 ya mwaka 2009, Kaimu Jaji Mkuu alisema sheria hii inashirikisha mihimili yote mitatu hivyo haki zote zinazotajwa na sheria hii ni lazima zipatikane inavyostahili. Prof. Juma pia amewataka Mahakimu wanaosikiliza kesi za watoto kuainisha mapungufu ya sheria hii na kuyawasilisha kwenye kamati ya Jaji Mkuu inayohusu masuala ya Sheria.
Aidha, Kaimu Jaji Mkuu amewataka Majaji na Mahakimu nchini wanaosikiliza kesi za watoto kujisomea zaidi masuala yanayohusu maendeleo ya haki za watoto kwa kuzisoma taarifa za utekelezaji za nchini pamoja na zile za nchi nyingine ili kupanua uelewa wa sheria hizo.
Kaimu Jaji Mkuu pia amewataka Majaji na Mahakimu wote kusimamia na kuhakikisha masuala yote yaliyotajwa na Sheria pamoja na mikataba ya kimataifa kuhusu watoto yanatekelezwa pindi wanapofanya ukaguzi kwenye magereza mbalimbali.
Wakati huo huo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali amewaomba UNICEF kufikiria na kuangalia uwezekano wa kujenga majengo mengine manne ya mahakama za watoto katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Tabora ili kuwapatia Mahakimu fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Mahakama za watoto zinavyofanya kazi.
Jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya lililojengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na UNICEF limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 415 ambapo Mahakama imechangia kiasi cha shilingi milioni 214 na UNICEF shilingi milioni 201.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni