Jumanne, 29 Agosti 2017

MTENDAJI WA MAHAKAMA MKOA WA PWANI ASTAAFU.


Na Rashid Haji, Mahakama, Pwani
Mtendaji Mstaafu wa Mahakama- Mkoa wa Pwani, Bw. Evarist Mmbagga amewasihi Watumishi wa Mahakama mkoani humo kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na ushirikiano ‘team work’ ili kuendelea kulipeleka gurudumu la maendeleo mbele.

Aliyasema hayo mapema wiki hii alipokuwa katika hafla fupi ya kuagwa na Watumishi wa Mahakama mkoani humo kufuatia kustaafu kwake baada ya kulitumikia taifa kwa zaidi ya miaka thelathini na tano.

“Licha ya changamoto za kiutendaji, nina imani kama Watumishi wa Mahakama mkiendelea kuchapa kazi kwa ushirikiano mtaiwezesha kuifikisha Mahakama mahali pazuri,” alisisitiza Bw. Mmbagga.

Aidha; Bw. Mmbagga aliwashukuru watumishi wote wa Mahakama mkoa wa Pwani na Mahakama ya Tanzania kwa ujumla kwa kumpa ushirikiano mkubwa wakati wa kutekeleza majukumu yake.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama wakimkabidhi zawadi Mtendaji Mstaafu wa Mahakama ya Mkoa-Pwani, Bw. Evarist Mmbagga (kulia) katika hafla fupi ya kumuaga aliyofanyiwa mapema wiki hii.
Zawadi  kwa Mtendaji Mstaafu (kushoto)
Watumishi wa Mahakama wakigonganisha glass na Mtendaji Mstaafu wa Mahakama ya Mkoa Pwani kama ishara ya kumtakia heri baada ya kustaafu rasmi.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni