Baadhi ya Maafisa
kutoka vitengo mbalimbali vya Mahakama wakiandaa Mpango wa Ununuzi wa Mahakama
kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kazi hiyo inafanyika katika Ukumbi wa Mahakama
Kuu-Divisheni ya Ardhi, wa kwanza kushoto ni Bw. Remigius R. Kyaruzi, Fedha na Uhasibu, katikati ni Bw. Prosper Munisi, Afisa Ugavi-Mahakama ya Tanzania, wa kwanza kushoto ni Bw. Ndezi Shiwa, Mkaguzi wa Ndani-Mahakama ya Tanzania.
Kazi ikiendelea, wa kwanza kushoto ni Bi. Scholastica Majinge, Afisa Ugavi-Mahakama Kuu ya Tanzania, katikati ni Bw. William Kimweri kutoka Kitengo cha Ugavi-Mahakama na wa kwanza kushoto ni Bw. Godlisten Mchaki, Afisa Ugavi-Mahakama Kuu-Divisheni ya Biashara.
Maafisa wakiendelea na kazi, wa kwanza kushoto ni Bw. Juma Hijja Kabogota, Afisa Ugavi-Mahakama ya Tanzania, wa kwanza kulia ni Bi. Edith Masuki, Afisa Ugavi-Mahakama katikati ni Bw. Audax Francis kutoka Idara ya Ununuzi na Ugavi-Mahakama ya Tanzania.
Mmoja wa washiriki wa Timu ya Kuandaa Mpango wa Ununuzi wa Mahakama, Bi. Peace Mpango-Mwanasheria wa Mahakama akiendelea na kazi hiyo.
Mpango wa Ununuzi unalenga katika kuwezesha kutekeleza Bajeti ya Taasisi kwa mwaka husika wa fedha, vilevile unawezesha kubaini njia za ununuzi zitakazotumika katika kununua vifaa/huduma husika.
Aidha Mpango wa Ununuzi unawezesha Idara/Vitengo kupata vifaa/huduma kwa wakati.
(Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni