|
Mtendaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Bw. Moses Mwidete wa pili kutoka
(kulia) akiwa na baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Mbeya, wakati wakiwa katika ziara ya kubadilisha uzoefu wa
utendaji kazi na changamoto wanazokabiliana nazo ili kuweza
kuongeza ubunifu na weledi wa kukabiliana nazo.
Aidha
Mtendaji huyo alililisifu jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, ambapo alisema
limekuwa msaada mkubwa kwa watumishi na jamii ikilinganishwa na jengo
lililokuwa likitumiwa hapo awali.
Aliongeza
kwamba jengo hilo, lina vyumba vikubwa mahakama za wazi na lina
mfumo imara wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA). Hivyo
aliwataka watumishi wa mahakama hiyo, kuendelea kulitunza ili
kuweza kutoa huduma bora na kwa wakati kama inavyoelekezwa katika
mpango makakati wa Mahakama ya Tanzania. (Picha na Rashid Omar ,
Pwani )
Mtendaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Bw. Moses Mwidete
amesema kwamba Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango
Makakati wa Miaka Mitano (2015/16 hadi 2019/20
inatarajia kujenga Mahakama ya Wilaya ya Chunya yenye
muonekano sambamba ya Mahakama ya Wilaya ya Kibaha. |
|
Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani
Tutindaga Mwankina (kulia) akiwakaribisha kwa furaha watumishi
kutoka Mahakama wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, wakati wakiwa katika
ziara ya kubadilisha uzoefu wa utendaji kazi.
|
|
Baadhi ya
Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na Dar es Salaam
wakibadilisha changamoto wanazokabiliana nazo
katika utendaji kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni