Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akisalimiana na Mhe. Benedict Mwingwa,Jaji-Mahakama Kuu ya Tanzania-Kanda ya Moshi, pindi alipopita katika Nyumba ya kulala Majaji 'Judges Lodge' mapema Septemba 14, kwa lengo la kuwajulia hali japo kwa muda mfupi akiwa njiani kuelekea Arusha kushiriki katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania utakaofanyika Septemba 15 na 16, 2017 jijini Arusha, anayepandisha ngazi ni Mhe. Aishiel Sumari, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Kanda ya Moshi, aliyesimama mwenye suti ya kijivu ni Mhe. Patricia Fikirini, Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Moshi pamoja na viongozi wengine wa Mahakama katika Kanda hiyo akiwemo Naibu Msajili, Mtendaji pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi.
Mhe. Jaji Mkuu akisalimiana na Mtendaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Moshi, Bw. Donald. F. Makawia
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisaini kitabu cha wageni pindi alipowasili katika Nyumba ya Majaji 'Judges Lodge' iliyopo Moshi kwa lengo la kuwajulia hali Watumishi wa Kanda ya Moshi ambao waliwakilishwa na Viongozi wao ambao ni Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo, Majaji wa Kanda hiyo, Naibu Msajili, Mtendaji na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa huo.
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu- Kanda ya Moshi, Mhe. Aishiel Sumari akiwatambulisha kwa Mhe. Jaji Mkuu baadhi ya Viongozi wa Mahakama (hawapo pichani) waliofika kumpokea pindi alipowasili katika eneo hilo, Watumishi/Viongozi hao ni pamoja na Majaji wawili (2) wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Naibu Msajili, Mtendaji na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mkoa huo.
Waheshimiwa wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani), wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Moshi, Mhe. Benedict Mwingwa, anayefuata ni Mhe. Patricia Fikirini, Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Moshi, anayefuata ni Mtendaji wa Mahakama-Kanda ya Moshi, Bw. Donald Makawia, kushoto kwake ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu-Kanda ya Moshi, Mhe. Bernard A. Mpepo na wa kwanza kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi-Moshi.
Mhe. Jaji Sumari akimshukuru Mhe. Jaji Mkuu kwa kupita kuwasalimia, mbali na kumshukuru, Mhe. Sumari pia alichukua nafasi hiyo kwa niaba yake, Majaji na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Moshi kumpongeza Mhe. Jaji Mkuu kwa kuteuliwa kwake na Mhe. Rais kushika nafasi hiyo.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni