Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno katika
kikao cha Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kikao hicho cha siku
mbili kimeanza kufanyika mapema Septemba 15 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa (AICC) uliopo jijini Arusha
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiendesha kikao cha Majaji Wajaji kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano (AICC) jijini Arusha, wanaoonekana katika picha (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda Iringa, Mhe. Mary Shangali, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein A. Kattanga na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati.
Baadhi ya Wahe. Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho.
Wahe Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho,wa kwanza kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, katikati ni Mhe. David Mrango, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Kanda ya Songea, na wa kwanza kushoto, ni Mhe. Firmin Matogolo, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Makaramba akichangia katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi unaofanyika jijini Arusha, lengo la Mkutano huo ni kujadiliana kwa pamoja juu usikilizaji wa kesi wa haraka na kuondoa mlundikano wa mashauri na hatimaye wananchi waweze kupata haki zao kwa wakati na hatimaye nguzo namba mbili ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya
Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati iweze kutekelezeka ipasavyo.
Msajili-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta akiwasilisha mada mbele ya Wahe. Majaji Wafawidhi (hawapo pichani)
Sehemu ya Wahe. Majaji Wafawidhi wakiwa katika Mkutano.
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein A. Kattanga (wa tatu kulia), Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati, Mtendaji, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Solanus Nyimbi pamoja na Wasajili wakiwa katika Mkutano wa Wahe. Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
(Picha na Mary Gwera,Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni