Pichani
ni muonekano wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania linajengwa
katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
linalojengwa chini ya Mradi wa Benki ya Dunia (WB), kwa sasa jengo hilo lipo
kwa hatua za mwisho za umalizwaji wa wake, ikiwa ni pamoja na uwekaji wa
marumaru (tiles), madirisha na milango, pia upakaji wa rangi.
Kazi ya uwekaji 'tiles'ikiendelea kama zinavyoonekana katika picha hapo juu.
Madirisha yakiwa tayari kuwekwa katika jengo hilo.
Pichani ni muonekano wa moja ya milango ambayo tayari imeshawekwa katika jengo hilo, kwa mujibu wa Mhandisi wa Moladi Tanzania, Eng.Steven Hanta amesema kuwa jengo hilo linatarajiwa kukamilika kati ya tarehe 06 mpaka 07, Oktoba, 2017 endapo hakutajitokeza tatizo lolote.
Kwa mujibu wa mpango uliopo jengo hilo linatarajiwa kufunguliwa rasmi sambasamba na kuanza rasmi kwa mafunzo ya kwanza Oktoba 12, 2017.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni