Na Mary Gwera, Mahakama
Mwakilishi ‘Practice Manager’ kutoka Benki ya Dunia (WB), Bw. George Larbi ameisifu Mahakama
kwa utekelezaji wake wa Mradi wa Maboresho wa huduma za Kimahakama.
Bw. Larbi
aliyasema hayo mapema Septemba 19, alipokutana na Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake
Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam ambapo alipata nafasi ya kuongea na Mhe. Jaji
Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama akiwemo Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania.
“Mradi
huu unaotekelezwa na Mahakama ni mradi wa mfano ambapo mafanikio yake
yanatarajiwa kuigwa na nchi nyingine,” alisema Bw. Larbi.
Bw. Larbi ambaye amewasili nchini kutokea Washington D.C zilipo ofisi za Benki ya Dunia amefanya ziara yake kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB).
Alisema Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama ni Mradi wa pili kwa nchi za Afrika ambapo Benki ya Dunia inashirikiana moja kwa moja na Mahakama katika kuboresha huduma ya utoaji haki.
Maeneo muhimu yanaotekelezwa na Mradi wa Benki ya Dunia (WB) ni pamoja na; Mapambano dhidi ya Rushwa; ni kwa jinsi gani Mahakama pamoja na wadau wengine wanaweza kushirikiana katika kupiga vita vitendo vya rushwa.
Maeneo mengine ni ushirikishaji wa wadau katika masuala yote ya utoaji haki na kusogeza huduma ya utoaji haki karibu na wananchi.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibarhim Hamis Juma (kulia) akiongea neno na Bw.
George Larbi kutoka Benki ya Dunia (katikati) wa kwanza kushoto ni Bw. Denis
Biseko 'Co-Team Task Leadear' wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Kimahakama.
Bw. George Larbi, kutoka Benki ya Dunia (WB) (katikati) akiongea na Mhe. Jaji Mkuu (kulia).
Mhe.
Jaji Mkuu (aliyeketi wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Wageni kutoka Benki ya
Dunia (wawili walioketi katikati) wa tatu kutoka kushoto ni Mtendaji
Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa pili kushoto ni Msajili
Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na wa kwanza kushoto ni Mkuu
wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho wa Huduma za Mahakama, Mhe. Zahra Maruma.
Ukaguzi:
Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mahakama cha Mahakama-Kisutu unaojengwa kwa fedha
za Benki ya Dunia
Bw.
George Larbi kutoka Benki ya Dunia pia alipata fursa ya kutembelea Mradi wa
ujenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Mahakama unaofanyika katika eneo la Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, kwa sasa kazi ya upakaji rangi katika jengo hilo
inaendelea.
Mafundi wakiendelea na kazi ya upakaji rangi katika jengo la Kituo cha Mafunzo linalojengwa Kisutu-Dar es Salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni