Jumatatu, 18 Septemba 2017

WATUMISHI WA MAHAKAMA YA UGANDA WATEMBELEA MAHAKAMA YA TANZANIA


Naibu  Msajili  wa Mahakama  Kuu  Divisheni  ya Makosa  ya  Rushwa  na Uhujumu Uchumi, Mhe. Charles Magesa, akielezea  jinsi  mifumo ya kielektroniki   ya kutunza  na jinsi Mahakama ya Tanzania  inavyotekeleza   shughuli mbalimbali. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mchumi  Mwandamizi  kutoka Mahakama Kuu ya  Uganda , Felix  Okurut (kushoto), ambaye pia anashughulikia  masuala  ya Mipango  na Maendeleo  akiangalia  moja ya kifaa ya kubebea majalada ya kesi  mbalimbali (reki) katika  Mahakama Kuu  - Divisheni  ya Ardhi, kulia  ni Naibu   Msajili  wa Mahakama  Kuu - Divisheni  ya Makosa ya Rushwa  na Uhujumu Uchumi,  Mhe. Charles Magesa.    Wageni wao pia walielezea jinsi Mahakama  za Uganda zinavyofanya kazi.
Baadhi ya wageni  kutoka  Mahakama Kuu  ya Uganda  waliotembelea  Mahakama Kuu – Divisheni  ya  Kazi iliyopo  jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia mifumo ya kielektroniki ya kuhifadhi na kutunza kumbukumbu  za  mashauri mbalimbali yaliyopo Mahakamani.
(Picha na Magreth  Kinabo)




         



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni