Mtendaji Mkuu-Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (katikati) na Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania,
Mhe. Katarina Revocati (kulia) wakimkabidhi
Msajili-Mahakama ya Rufani (T), Mhe. John Kahyoza,Mkataba wa kazi wa
Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Mahakama (2015/16-2019/20).
Zoezi
hilo la kutia saini na kukabidhiana Mikataba hiyo limefanyika katika Ukumbi wa
Maktaba (Mahakama ya Rufani) huku kwa baadhi ya Wakuu wa Idara ikiwa ni pamoja
na Mkurugenzi Msaidizi Tehama (DICT), Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na
Mawasiliano (HoIECU) na Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi na Majengo –Mahakama ya
Tanzania (HEM) Wakuu wengine wa Vitengona Idara watakabidhiwa Mikataba hiyo
wiki ijayo.
Mkurugenzi Msaidizi-TEHAMA, Mahakama ya Tanzania, Bw. Machumu Essaba (kushoto) akikabidhiwa Mkataba wa Kazi na Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (katikati), kulia ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati.
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe (kushoto) akikabidhiwa Mkataba wa kazi kwa ajili ya utekelezaji kwa mwaka 2017/2018.
Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi na Majengo-Mahakama ya Tanzania, Mhandisi. Khamadu Kitunzi (kushoto) akikabidhiwa Mkataba wa Kazi kwa ajili ya utekelezaji.
(Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni