Ijumaa, 29 Septemba 2017

WANASHERIA WA UMOJA WA 'PAN- AFRICAN' WAMTEMBELEA JAJI MKUU

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na wanasheria kutoka Umoja wa Wanasheria wa Pan-African (Pan-Africam Lawyers Union) waliofika Ofisini kwake kumtembelea leo jijini Dar es salaam. Katika Mazungumzo yao, Jaji Mkuu alisema anatambua mchango wa Taasisi hiyo pamoja na Taasisi nyingine za Kisheria katika kuzungumzia masuala yanayowahusu wanasheria. Wanasheria hao wanatoka katika nchi za Zambia, Kenya, Uganda,
Cameroon na Tunisia.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na wanasheria kutoka Umoja wa Wanasheria wa Pan-African (Pan-Africam Lawyers Union), (hawapo pichani) waliofika kumtembelea ofisini kwake, leo jijini Dar es salaam. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na wanasheria kutoka Umoja wa Wanasheria wa Pan-African (Pan-African Lawyers Union), waliofika kumtembelea ofisini kwake, leo jijini Dar es salaam. Wa pili kushoto ni Rais wa Umoja huo, Mhe. Elijah Banda ambaye anatoka nchini Zambia.
 
(Picha na Lydia Churi)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni