Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma amewataka wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto kujiendeleza katika fani ya Sheria kwa kuwa na hitaji na hamu ya kujiendeleza zaidi toka kiwango
kimoja cha elimu hadi cha juu zaidi.
Prof. Juma ameyasema
hayo mjini Lushoto katika mahafali ya 17 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama ambapo
wahitimu 150 walitunukiwa Stashahada ya Sheria na wengine 142 walitunukiwa Astashahada ya Sheria.
Amesema kwamba wahitimu
hao na wasomi wengine wa sheria nchini hawana budi kuzingatia kasi ya sasa ya
maendeleo ya dunia na umuhimu wa elimu katika ulimwengu wa leo na kongeza kwa
kutokana na hali hiyo ni lazima wajiendeleze zaidi katika fani hiyo.
“ Ninawaasa popote pale
mtakapokuwa someni na kujiendeeleza na jifunzeni
mambo mapya kila siku, karne hii ya 21 ni karne ya teknolojia na habari
, ni karne inayowategemea wahitimu wanaojiendeleza na kujifunza kila siku, jiendelezeni hadi kufikia
viwango vya juu kulingana na kushindana na yeyote yule duniani , kumbukeni kuwa
ajifunzae haachi kujua, naomba mtambue kuwa kujifunza ni kwekeza,” alisisitiza
Jaji Mkuu.
Mhe. Jaji Mkuu pia
amewaasa wahitimu hao kuwa watakapopata kazi wahakikishe wanafanya kazi kwa bidii,
uaminifu na kwa wakati ili kulinda maslahi ya Taifa na hivyo kuwa mabalozi
wazuri wa Chuo.
Awali akimkaribisha
Jaji Mkuu katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Jaji Mstaafu
wa Mahakama ya Rufaa Mhe. John Mrosso amesema ndani ya miaka miwili chuo
kimepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kujielekeza katika masuala ya
utafiti na ushauri ambapo inao wanataaluma 22 ambao wamejikita katika eneo hilo
na kuwezasha wahitimu wa chuo hicho kupata ajira serikalini na kubuni vyanzo
mbalimbali vya mapato ili kujiendesha.
Nae Mkuu wa Chuo hicha
Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo alisema katika mwaka huu chuo kimefanikiwa kutoa
wanafunzi 26 waliopata daraja la kwanza hali ambayo imetokana na kujitoa kwa
wahadhiri na kujituma kawa wanachuo hao na hivyo kukiletea sifa chuo.
Amesema kama chuo
wamepanga kuimarisha kitengo cha mafunzo, kuimarisha vyanzo vya mapato, kujenga
uwezo wa watumishi ili kuhakikisha kinatekeleza kwa vitendo dhamira ya
kuanzishwa kwa chuo ya kuboresha utendaji kazi
wa Mahakama kupitia mafunzo kwa Maafisa wa Mahakama pamoja na wasaidizi
wao na wadau wote wa sekta ya sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
Khamis Juma akizungumza na wahatimu na wageni waalikwa katika mahafali ya 17 ya
chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto ambapo wahitimu 292 walitunukiwa
Stashahada na Astashahada za Sheria.
Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Mst. wa
Mahakama ya Rufaa Mhe.John Mrosso akizngumza wakati wa Mahafali ya 17 ya
Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Mkuu wa
Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Dkt. Paul Kihwelo akizungumza kitu
wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho pembeni yake ni a na mgeni rasmi
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma
Baadhi ya
Wahitimu wa Stashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa
mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Stashahada zao.
Baadhi ya
Wahitimu wa Astashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa
mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Astashahada zao.
Jaji Mkuu
wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Jarida la Chuo cha
Uongozi wa Mahakama Lushoto wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni