Jumanne, 28 Novemba 2017

JAJI MKUU WA TANZANIA AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akiwa na ujumbe wake kutoka Mahakama ya Tanzania ofisini kwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Novemba, 27, 2017 alipokwenda kujitambulisha rasmi kwa Rais huyo. Anayefuatia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akifuatiwa na Msajili Mkuu, Mhe. Katarina Revokati.
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na ujumbe ulifuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania ofisini kwake Zanzibar baada ya Jaji Mkuu kwenda kujitambulisha rasmi.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein jana alipokwenda kujitambulisha rasmi kwa Rais huyo. 
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi  jana alipokwenda kujitambulisha rasmi kwa Rais huyo. 
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipokwenda kujitambulisha kwa Rais huyo jana mjini Zanzibar.  Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuelezea jambo Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein alipomtembelea ofisini kwake jana.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Mahakama ya Tanzania ukiongozwa na Jaji Mkuu walipomtembelea jana ofisini kwake Zanzibar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni