Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Waleed Malik akiwa na wenzake walipofika ofisini kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga. Wawakilishi hao kutoka Benki ya Dunia wako nchini kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama pamoja na Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/2010) wa Mahakama.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akizungumza na wataalamu kutoka Benki ya Dunia wakiongozwa na Waleed Malik waliofika nchini kwa ajili ya kukagua shughuli za utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama pamoja na Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/2010) wa Mahakama.
Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Waleed Malik akizungumza.
Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Waleed Malik akibadilishana mawazo na viongozi wa Mahakama ya Tanzania. Katikati ni Msajili Mkuu Mhe. Katarina Revokati.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga( wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wenzake pamoja na wageni kutoka Benki ya Dunia. Wa kwanza kulia ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Waleed Malik akifuatiwa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati. Wa pili kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama Mhe. Zahra Maruma.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati akiwa na Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama Mhe. Zahara Maruma.
Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Waleed Malik akiwa na wenzake akizungumza leo jijini Dar es salaam alipokuwa ofisini kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga kwa ajili ya kujadili utekelezaji utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama pamoja na Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/2010) wa Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni