Jumanne, 5 Desemba 2017

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA NA WIZARA YA ARDHI ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO

Na Lydia Churi
Mahakama Kuu ya Tanzania pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo wamesaini Hati ya Makubaliano (Memorundum of Understanding) yatakayowezesha upatikanaji wa haraka wa nyaraka kutoka kwenye Mabaraza ya Ardhi.  

Hati hiyo ya Makubaliano ilisainiwa na pande zote mbili ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika alisaini kwa niaba ya wizara yake na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ilvin Mugeta alisaini kwa niaba ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kusainiwa kwa hati hiyo ya Makubaliano kutaiwezesha Mahakama Kuu ya Tanzania kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa nyaraka kutoka kwenye Mabaraza ya Ardhi nchini. 

Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ilvin Mugeta (kushoto) akisaini Hati ya Makubaliano kati ya Mahakama Kuu ya Tanzania na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo jijini Dar es salaam. Hati hiyo itawezesha upatikanaji wa haraka wa nyaraka kutoka kwenye Mabaraza ya Ardhi. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika.

Kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo ya muda mrefu ya upatikanaji wanyaraka zinazohitajika katika shughuli za Mahakama, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Mahakama Kuu ya Tanzania walifanya vikao vya mashauriano mwezi Machi na April ili kutatua tatizo hilo.

Aidha, Hati hiyo ya Makubaliano imeainisha maeneo ya ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi kuwa ni kujengeana uwezo pamoja na vitendea kazi.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika akisaini Hati ya Makubaliano kati ya Mahakama Kuu ya Tanzania na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo jijini Dar es salaam. Hati hiyo itawezesha upatikanaji wa haraka wa nyaraka kutoka kwenye Mabaraza ya Ardhi. 

Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ilvin Mugeta (kushoto) akipokea  Hati ya Makubaliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika leo jijini Dar es salaam. 

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bwana Leonard Magacha (waliosimama wa kwanza kulia)  akifuatiwa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ilvin Mugeta wakishuhudia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika akisaini Hati ya Makubaliano kati ya Mahakama Kuu ya Tanzania na Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam. 













Hakuna maoni:

Chapisha Maoni