Baadhi
ya Wasaidizi wa kisheria
wakichambua vielelezo
mbalimbali katika Wiki ya Msaada wa Kisheria
inayoendelea katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja Jijini Dar
es Salaam.
|
Mwakili wa kujitegemea Job
Kerario (kulia ) akitoa msaada wa
kisheria kwa Mama Riziki
Shah ambaye anataka msaada wa
kisheria baada ya kufika kwenye Wiki
ya Msaada wa Kisheria inayoendelea kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja , jijini Dar es Salaam baada ya kukosa Matunzo kwa Mumewe.
Na Magreth Kinabo – Mahakama
Kituo cha Msaada wa Kisheria kijulikanacho
kwa jina la Paralegal
kimewashauri wananchi wenye nia ya kununua viwanja kufika katika Manispaa
husika ili kuweza kuepukana na tatizo la migogoro ya Ardhi
na kuepusha upotevu wa rasilimali
fedha wanazozitumia.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 6,
Desemba 2017 na Katibu
wa kituo hicho, Antony Isakwi katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es salaam ambapo Maonesho ya Wiki ya
Msaada wa Kisheria yanaendelea.
“Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba wanatakiwa kununua ardhi baada ya
kupata maelekezo sahihi
kutoka katika Manispaa
husika badala ya kununua
ardhi kiholela, kwa kuwa kwa kufanya
hivyo itasaidia kuepusha kupoteza fedha kwa kununua
ardhi kwenye maeneo yasiyo
sahihi,”alisema Isakwi.
Wiki hiyo ya kisheria iliyoanza rasmi
Desemba 4, na inatarajiwa kumalizika
Desemba 8, mwaka huu, ambapo Katibu huyo alisema
bado kuna umuhimu mkubwa wa kuwaelimisha wananchi ili kuweza kuepukana
na tatizo hilo, pamoja na matatizo mengine kama vile ukatili wa kijinsia,
mirathi na matunzo kwa watoto.
Alisema
kituo chake kimeweza kuwapokea wananchi zaidi ya 50 waliokuwa
wakihitaji msaada wa kisheria
tangu walipoanza huduma hiyo, ambayo
wanaitoa bure kwenye viwanja hivyo. Aidha
kituo hicho pia kimeshawapatia wananchi wanaohitaji huduma ya kisheria wapatao 360,000 katika kipindi cha mwaka
mwaka huu. Aliongeza kuwa idadi
kubwa ya watu walijitokeza katika kituo hicho ni wale wenye matatizo ya migogoro ya ardhi, kijinsia,
mirathi na matatizo ya matunzo kwa watoto.
Kwa upande wake
Msaidizi wa kisheria Athuman Maghembe
aliviasa vyombo vya habari
nchini kutumia nafasi hiyo kwa
kuelimisha watanzania umuhimu wa
wiki hiyo ili waweze kuepukana na
matatizo hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni