Jaji Kiongozi Mahakama Kuu
ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (kulia) akimuonyesha Naibu Jaji Mkuu wa Namibia (katikati anayetazama juu), Mhe.
Petrus Damaseb moja ya Kumbi za
Mahakama Kuu, Naibu huyo Jaji Mkuu pamoja na ujumbe alioambatana nao
wametembelea Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kujifunza na kubadilishana
uzoefu wa uendeshaji wa Mahakama hususani Suala la utoaji haki ambalo ndio jukumu
kuu la Mahakama. Aidha Naibu Jaji Mkuu huyo atatembelea pia Mahakama Kuu-Divisheni ya Biashara mapema Desemba 08.
Jaji Kiongozi-Mahakama
Kuu ya Tanzania (kushoto) akimuonyesha, Naibu Jaji Mkuu wa Namibia Mhe. Petrus
Damaseb Maktaba ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Picha ya pamoja: Jaji
Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) pamoja na
Naibu Jaji Mkuu wa Namibia (wa nne kushoto) wakiwa katika picha mara baada ya
kumaliza maongezi.
Mkuu
wa Kitengo cha Usimamizi wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama (JDU) Mhe. Zahra
Maruma, akiwasilisha Mada mbele ya Naibu Jaji Mkuu wa Namibia na Ujumbe
alioambatana nao, Mhe. Maruma aliwasilisha mada ya jinsi Mahakama
inavyotekeleza Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (5) (2015/2016-2019/2020),
ikiwa ni pamoja na mafanikio na changamoto.
Jaji
Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akichangia mada, kushoto ni Naibu
Jaji Mkuu wa Namibia Mhe. Petrus Damaseb akimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Kiongozi.
Naibu
Jaji Mkuu wa Namibia, Mhe. Petrus Damaseb akichangia: Mhe.
Damaseb ametoa uzoefu wa Mahakama- Namibia hususani katika Suala la hukumu
zinazotolewa na Wahe. Majaji ambapo amesema kuwa pindi Jaji husika anapomaliza
kesi hutakiwa kuwasilisha ‘summary’ ya hukumu aliyoitoa ili iweze kuwekwa
katika tovuti kwa ajili ya kuwezesha Wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Mawakili kupata elimu/rejea.
Msajili
Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati akichangia jambo katika
kikao hicho, Mhe. Revokati aliuomba Ujumbe huo kutoka Namibia kutoa uzoefu wao
katika masuala mbalimbali hususani ni jinsi gani wanafanya katika utoaji wa ‘Law
Reports’ na masuala mengineyo, kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Amir R. Mruma.
Baadhi ya Wajumbe
wakifuatilia na kusikiliza kwa umakini mada iliyokuwa ikitolewa, wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Amir Mruma, (wa pili
kushoto) ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa
kwanza kushoto ni Msajili-Mahakama ya Rufani (T), Mhe. John Kahyoza, wa tatu ni
Mtendaji-Mahakama ya Rufani (T)- Mhe. Sollanus Nyimbi na wa pili kulia ni
Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati na wa tatu kulia ni Mhe. Ndunguru, Katibu wa Mhe. Jaji Kiongozi.
(Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni