Na Magreth Kinabo
Waziri wa Katiba na
Sheria, Profesa amesema kwamba
bado changamoto ya uhitaji mkubwa
ujenzi na ukarabati miundombinu ya
Mahakama nchini.
Kauli hiyo ilitolewa leo na wakati akizindua wa Mahakama ya
Wilaya Kigamboni, iliyopo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya mkakati wa Mahakama wa kukabiliana na changamoto hiyo.
“ Ni ukweli usiopingika
kuwa tuna changamoto kubwa ya miundombinu ya Mahakama hapa nchini. Hadi kufikia mwaka
jana tulikuwa tunahitaji kujenga Mahakama kuu
19, Mahakama Hakimu Mkazi 14, Mahakama za Wilaya 109 na mahakama za
mwanzo 3003’’, alisema Waziri huyo.
Aliongeza kwamba tukio
hilo linampa faraja
kwa kuwa linatatua moja ya
changamoto kubwa inayoikabili Mahakama
na Sekta ya Sheria kwa ujumla.
Profesa Kabudi
alifafanua kwamba katika hali iliyopo ya
mahitaji makubwa ya ujenzi na ukarabati wa Mahakama nchini ubunifu, umakini na kuweka
vipaumbele katika kujikwamua na hali iliyopo.
Hata hivyo Profesa
Kabudi aliupongeza uongozi wa Mahakama
kwa kuwa wabunifu na kufanya tafiti ya teknolojia ya gharama nafuu katika ujenzi iitayo
Moladi kwa ajili ya kutumia na
kujengea majengo ya Mahakama,
“Nimetembelea majengo
haya ya mahakama nimeridhishwa na viwango vya ubora majengo haya.
Teknolojia hii sio tu
inapunguza gharama za ujenzi,
bali pia inapunguza muda wa ujenzi. Faida hizo
zinawezesha fedha nyingine kutumika katika kujenga au kukarabati majengo
mengine,” alisisitiza.
Alisema Serikali inatambua jukumu la kutenda haki haliwezi kuwa la
ufanisi pasipo miundombinu ya kisasa na inayokidhi vigezo vya eneo husika.
Alitoa wito kwa Mahakama kuendelea kushauriana na Serikali
ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea
ya kupanua wigo wa upatikanaji wa haki
kwa kujenga na kukarabati Mahakama zetu.
Aidha Profesa
aliwata watumishi na watumiaji wa
mahakama hiyo kuitunza miundombinu waliojengewa
ili iweze kudumu kwa muda mrefu.Kwa upande wake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu aliutaka uongozi wa wilaya hiyo uanze kufikiria eneo lingine la ujenzi wa mahakama nyingine.
Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni pamoja na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni.
Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza kabla ya kuzindua Mahakama mpya ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Mahakama. Kulia kwake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kushoto kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akifuatiwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam Mhe. Beatrice Mutungi.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akipanda Mti baada ya kuzinduliwa kwa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam.
(picha na Lydia
Churi )
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni