Kauli hiyo
ilitolewa leo na Jaji Kiongozi huyo wakati akifungua Kongamano la
Mazungumzo ya wadau kujadili rasimu ya mtaala
wa mafunzo kwa Madalali wa Mahakama na Wanaopeleka hati za Mahakama yanayoendelea katika Kituo cha Mafunzo Kisutu, jijini Dar
es Salaam.
Jaji
kiongozi huyo , amewataka wadau wa
Mahakama kuweka kipaumbele suala la elimu
kwa madalali ikiwa ni njia
mojawapo ya kuongeza ujuzi na kuhakikisha
wanafanyakazi kwa weledi na maadili
yanayotakiwa.
“Ni suala
lisiloweza kubishaniwa na yeyote mwenye ufahamu wa elimu kuwa ni muhimu kuendelea
kujifunza kwani huwezi kujua kila kitu,” alisisitiza Wambali.
Aliongeza kwamba suala la kujifunza siku zote
lazima lipewe kipaumbele na kilammoja katika fani hii muhimu na nyingine.
Aidha Wambali
aliongeza kwamba madalali wa Mahakama
na wale wanaopaswa kupeleka hati
za kuitwa kwenye mashauri
wanaowajibu mkubwa katika kuhakikisha
kuwa amri mbalimbali zinazotolewa na Mahakama hususani katika mashauri ya madai zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni
zilizowekwa.
“ Kwa hali hiyo
, kazi ya utekelezaji wa amri za mahakama inatakiwa kuhudumiwa
au kuongozwa na watu wenye uaminifu, maadili ya hali ya juu, bali pia
wenye ujuzi na upeo na uzoefu wa hali ya
Juu kuhusu sheria na kanuni zinazohusu
upelekaji taarifa, uendeshaji
mashauri na utekelezaji wa maamuzi.
Alisema pamoja
na ukweli kuwa mwaka 1997 zilitungwa
kanuni kuhusu uteuzi, maslahi na usimamizi wa madalali wa Mahakama na wengi wa
madalali waliendelea kuifanya
kazi yao , bado hakukuwahi kuwa
na mafunzo yoyote rasmi ya
kuwafanya wapate ujuzi zaidi wa
utekelezaji wa kazi zao ukiacha yale ya
dharura yaliyofanyika mwaka 2003 kwa
wale wa Dar es Salaam na Mtwara.
Hali hiyo
ilisababisha malalamiko
mengi kutoka kwa wadaawa na umma kwa ujumla
kuhusu mapungufu yaliyojitokeza ikiwemo ukiukwaji wa taratibu na ukosefu wa maadili katika
utekelezaji wa majukumu ya madalali.
Wambali alifafanua kwamba kutokana na changamoto
kadhaa Mahakama ilifanya marekebisho kuhusu namna ya kuwapata madalali, kusimamia nidhamu na maadili , maslahi na jinsi ya
kutekeleza majukumu yao. Ni kwa sababu hiyo Sheria (Taarifa ya Serikali
namba 363 ya 2017)ilitungwa na
kuchapishwa tarehe 22/9/2017 hivyo
,sheria hiyo imefuta ya sheria ya 1997.
“ Ni matumaini
yangu kuwa sheria hii itakuwa
muarobani wa changamoto nyingi
zilizokuwa zimejitokeza badala ya kuwa ni kikwazo cha mabadiliko.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama(IJA) Dkt. Paul Kihwelo
alisema ili kuondokana na lawama za
madalali ambazo kimsingi zilikuwa
zikirejeshwa kwa Mahakama , Mahakama iliamua kutunga kanuni mpya za 2017 zinazosimamia shughuli za na
wasambaza wito.
Pamoja na
mambo mengine kanuni hizo mpya zimeongeza mambo mawili ; imetenganisha Dalali wa Mahakama na Msambaza Wito na Amri za
Mahakama.
Dkt. Paul alisema kila mtu anayekidhi vigezo vya kuwa dalali, au msambaza wito na amri za mahakama apate Cheti cha Uthibitisho kutoka
Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto ama chuo kingine kinachotambuliwa na Kamati
ya Nidhamu na Uteuzi wa Madalali na Wasambaza wito na Amri
za Mahakama ambayo mwenyekiti wake
ni Mheshimiwa Jaji Kiongozi
Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinad Wambali akitoa hotuba katika Kongamano
hilo.
|
|
|
Baadhi ya wadau wa mkutano wa Kongamano la kujadili rasimu ya mtaala wa mafunzo kwa madalali wakiwa katika
kongamano hilo na siku mbili. |
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinad Wambali(wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mahakama mara baada ya kufungua Kongamano hilo. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni