Na
Lydia Churi-Tabora
Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo nchini
kusimamia mabaraza ya kata yaliyoanzishwa kwa Shjeria yam waka 1985 kwa kuwa
mabaraza hayo ni sehemu muhimu katika mfumo wa utoaji haki kutokana na kazi
yake ya kusuluhisha na kupatanisha
mashauri madogo madogo ya jinai na madai.
Akizungumza na Watumishi
wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga na Nzega pamoja na Mahakama ya Mwanzo ya Ziba
na Nyasa mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema mfumo wa utoaji haki kupitia mabaraza
ya kata unawaunganisha wananchi tofauti na pale kesi inaposikilizwa Mahakamani
ambapo mar azote aliyeshindwa hujenga uadui na aliyeshinda.
Jaji Mkuu amesema endapo
mabaraza ya Kata yatasimamiwa ipasavyo ni wazi kuwa idadi ya kesi
zinazofunguliwa kwenye Mahakama za Mwanzo nchini itapungua kwa kiasi kikubwa
kwa kuwa kesi nyingi zitaamuliwa kwenye mabaraza hayo kwa njia ya usuluhishi na
upatanishi. Aliongeza kuwa kesi zote zinazosajiliwa nchini asilimia 74 ni za
Mahakama za Mwanzo.
Amesema ili kuimarisha
mfumo wa utoaji haki kupitia mabaraza ya kata, Mahakama ya Tanzania imeandaa
mpango wa mafunzo utakaowakutanisha Mahakimu pamoja na wajumbe wa mabaraza ya
kata.
Aidha, Prof. Juma
amewataka watumishi wa Mahakama
kuzingatia maadili ya kazi na kutoa haki kwa wakati kwa kuwa kwa kufanya hivyo
watachangia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Amesema mashauri
yanapomalizika kwa wakati hutoa nafasi kwa wananchi kufanya shughuli za
uzalishaji wa mali na hivyo kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.
“Mnapofanya kazi ya
utoaji wa haki mjisikie ni sehemu ya kujenga uchumi maana bila ya haki hakuna
amani”, alisema Prof. Juma na kuongeza kuwa Mahakama ina mchango mkubwa katika
kudumisha Amani, utulivu na umoja ambayo ni sehemu ya Dira ya Taifa yam waka
2025.
Akizungumzia matumizi ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ndani ya Mahakama, Jaji Mkuu amesema tayari
Mahakama imeshaanza kutumia mfumo huo kwa kukusanya takwimu za mashauri kuanzia
ngazi ya Mahakama za wilaya na pia baadhi ya majengo ya Mahakama tayari
yanatumia TEHAMA huku akitolea mfano jingo la Mahakama Kuu kanda ya Mbeya na
kituo cha Mafunzo Kisutu.
Amewataka watumishi wa
Mahakama wa kada zote kujiendeleza hasa katika matumizi ya Tehama ili Mahakama
iytekeleze wajibu wake wa kutoa haki kwa wakati. Amesema, kupitia Tehama
mahakama itatoa haki kwa haraka na kwa wakakti
hivyo wananchi wataongeza Imani yao kwa mhimili huo.
Mahakama katika katika
wilaya za Nzega, Igunga pamoja na Mahakama za Mwanzo Jaji Mkuu wa Tanzania
ameanza ziara ya kikazi Mahakama Kuu kanda ya Tabora ambayo inajumuisha mikoa
ya Tabora na Kigoma. Leo amekagua shughuli za za Ziba na Nyasa zilizopo mkoani
Tabora.
Jaji Mkuu wa Tanzania wa Tanzania Mhe, Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na wa Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega mara baada ya kuwasili ili kukagua shughjuli za Mahakama. Jaji Mkuu ameanza ziara Mahakama Kuu kanda ya Tabora.
Jaji Mkuu wa Tanzania wa Tanzania Mhe,Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni.
Jaji Mkuu wa Tanzania wa Tanzania Mhe,Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na watumishi Mahakama ya Wilaya ya Nzega mara baada ya kuwasili ili kukagua shughjuli za Mahakama. Jaji Mkuu ameanza ziara Mahakama Kuu kanda ya Tabora.
Jaji Mkuu wa Tanzania wa Tanzania Mhe,Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula alipowasili ofosini kwa Mkuu huyo wa wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula akizungumza.
Jaji Mkuu wa Tanzania wa Tanzania Mhe,Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Mkuu wawilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula kitabu kinachoelezea Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Jarida la Mahakama.
Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga wakimsikiliza Jaji Mkuu alipozungumza nao.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Tabora Mhe. Sam Rumanyika akizungungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga.
Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Ziba wakimsikiliza Mhe Jaji Mkuu ( hayupo Pichani) alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Ziba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni