Na Nurdin Ndimbe, Lindi
Katika kutekeleza dhamira yake ya kuboresha huduma za Mahakama na
kusogeza huduma hizo karibu zaidi na wananchi, Mahakama ya Tanzania kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia imeanza rasmi ujenzi wa majengo matatu ya
Mahakama katika mkoa wa Lindi pamoja na wilaya zake za Kilwa na Ruangwa
Ujenzi
wa Mahakama hizi ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2015/16 hadi
2019/2020) wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za
Mahakama ambao ulianza kutekelezwa rasmi mwaka 2015. Miradi hii kwa pamoja
inalenga kuboresha huduma na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Mahakama
imeanza ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mkoa wa Lindi ambalo litajumuisha pia na
Mahakama ya wilaya ya Lindi Majengo mengine yanayojengwa ni ya Mahakama za
wilaya za Kilwa na Ruangwa. Akizungumza na mwandishi wa habari hii Mtendaji wa
Mahakama Mkoani Lindi, Bw. Joseph Chota alisema kuwa miradi yote hii inajengwa na
Kampuni ya Moladi Tanzania. ‘’Unajua Mkoa wetu una matatizo makuwa ya
Miundombinu ya Mahakama, sehemu nyingi majengo sio ya kwetu aidha tumeazimwa au
kupewa na Halmashauri husika na majengo
haya ni ya siku nyingi na chakavu sana’’ alisema Mtendaji huyo. ‘’Kwa hiyo ujio
wa miradi mitatu ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kilwa, Ruangwa pamoja na jengo
la Mhakama ya Hakimu Mkazi Lindi ni faraja kubwa kwetu kwa Mahakama pamoja na Mkoa kwa ujumla’’
alisistiza.
Kwa upande wake Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Moladi Tanzania
inayosimamia ujenzi wa majengo hayo Mkoani Lindi Mhandisi Avkado amesema kuwa Mahakama
zote tatu zinajengwa na Kampuni ya Moladi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha
Ardhi.
“Kama mnavyoona Mahakama hizi zipo
katika hatua mbalimbali za ujenzi, kwa hapa Kilwa tayari zege la msingi
tumemaliza tunasubiri kuanza sasa kusimamisha
‘pannels’ kwa ajili ya kumwaga kuta za jengo lenyewe” Alisema Mhandisi
huyo.
Kuhusu ujenzi wa jengo la Mahakama
ya Hakimu Mkazi Lindi tuna changamoto ya udongo katika eneo la ujenzi hata
hivyo changamoto inashughulikiwa ili kupata ufumbuzi wa haraka ili tuendelee na
ujenzi.
“Mafanikio makubwa ya miradi hii iko
kwa upande wa mradi wetu Wilayani Ruangwa kwa sasa boma kwa maana ya jengo liko
tayari na sasa tumeanza kuunganisha vyuma kwa ajili kuanza kupaua jengo hilo, ukiancha
changamoto ndogondogo zinazojitokeza tunajitahidi kuhakikisha kuwa miradi hii
inamalizika katika muda uliopangwa,” alisistiza.
Katika mahojiano maalum na Hakimu wa Mahakama
ya Wilaya Ruangwa, Mhe.Ramla Shehagilo yaliyofanyika ofisini kwake Mahakama
ya Wilaya Ruangwa anasema kuwa ujenzi wa Mahakama hiyo unaoendelea katika Wilaya
hiyo umeleta faraja na ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo kwani
wamekuwa wakisumbuka kupata huduma katika jengo na mazingira yasiyo ya
kuridhisha.
“Kwakweli
wananchi wa Wilaya hii na hata wateja wanaokuja
katika Mahakama yetu wanaonekana kufurahia ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ambapo
pindi itakapokamilika itawaondolea adha ya kupata haki katika mazingira yasiyo
nadhifu, kama unavyoona jengo hili lilikuwa la Mahakama ya Mwanzo Ruangwa, ilipoanzishwa
Wilaya, Mahakama ya Wilaya ikaanzishwa kwahiyo tunafanyia kazi katika mazingira
magumu na ya kubanana” alisema Hakimu huyo wa Wilaya.
Azma ya Mahakama ya Tanzania ni kusambaza
huduma za Mahakama nchi nzima ili hata mwananchi aliyepo katika ngazi ya Kata
aweze kupata huduma ya Haki.
Mbali
na ujenzi pia kumekuwa na ukarabati wa majengo ya Mahakama ya mara kwa mara zote
zikiwa ni jitihada za kuhakikisha kunakuwa na miundombinu ya majengo bora ya
kutolea haki kama sehemu ya utekelezaji wa malengo yaliwekwa katika kutekeleza
uboreshaji wa Miundombinu na Mpango Mkakati ya Miaka mitano wa Mahakama.
Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Ruangwa Mhe.Ramla Shehagilo akitoa maelezo ya
maendeleo shughuli za Kimahakama pamoja na ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya
Ruangwa.
Muonekano
wa jengo hilo kwa upande wa mapana upande wa nyuma.
Jengo
la Mahakama ya Wilaya Ruangwa likionekana kwa juu likiwa tayari kuanza
kupauliwa.
Muonekano wa mbele wa jengo
Mtendaji wa Mahakama Mkoani Lindi
Bw Joseph Chota akiangalia msingi kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Hakimu
Kazi Lindi.Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi itakapokamilika itaghatimu milioni
642,490,000/-
Mwakilishi wa Kampuni ya Moladi
Tanzania Mhandisi Avcado akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Mahakama ya
Wilaya ya Kilwa mjini Kilwa Masoko.
Msingi uliochimbwa kwa ajili ya
kuanza ujenzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni