Na
Lydia Churi
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali amewataka watumishi
wa Mahakama pamoja na wadau wake wanaohusika na utatuzi wa migogoro ya kikazi
kushirikiana na kuimarisha maadili ya kitaaluma ili kuondokana na malalamiko kuhusu
rushwa.
Akifungua
Mkutano wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi pamoja na wadau wake leo jijini Dar
es salaam, Jaji Wambali alisema Watumishi wa Mahakama pamoja na wadau wanapaswa
kufahamu kuwa wanalo jukumu kubwa la kutoa haki kwa wakati, kwa ubora na kwa
weledi wa hali juu ili wawe ni sehemu ya furaha kwa wale wanaofika kupata
huduma.
Aidha,
Jaji kiongozi aliwataka watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi pamoja na
wadau wake kushirikiana katika kutatua migogoro ya kikazi ili kujenga Taswira nzuri kwa Mahakama.
Akizungumzia
kasi ya utatuzi wa migogoro ya kazi na utoaji wa haki, Jaji Wambali alizitaja
sababu zinazorudisha nyuma kasi hiyo kuwa ni umakini mdogo wa uandaaji wa nyaraka
mbalimbali zinazowasilishwa Mahakamani kwani kwa kutokuwa makini kumesababisha
migogoro mingi ya kazi kuchelewa kumalizika.
Alizitaja
sababu nyingine kuwa ni pamoja na Waajiri na waajiriwa kutumia wawakilishi wenye
uwezo mdogo, na kutuma wawakilishi wasiokuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi.
Baadhi
ya wadau wa Mahakama katika utatuzi wa migogoro ya kazi ni pamoja na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Ofisi
ya Kamishna wa Kazi, Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE), Vyama vya Wafanyakazi vikiongozwa na Shirikisho lao-(TUCTA,
Mawakili, na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Wakati
huo huo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya
watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa Alex amewataka wadau pamoja na Mahakama
Kuu Divisheni ya Kazi kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati ili kuvutia
wawekezaji, kuongeza tija mahala pa kazi na kukuza uchumi wa nchi.
“Kukua
kwa uchumi wa viwanda kutachochewa na
nguvu kazi yenye ujuzi inayofanya kazi kwa utulivu pasipokuwa na migogoro ya
kikazi, hivyo kuwepo kwa amani na utulivu kutasaidia kupunguza migogoro mahala
pa kazi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwa wingi, alisema Naibu
Waziri huyo.
Akizungumzia
kasi ya usikilizwaji wa mashauri, Mhe. Naibu Waziri alimuomba Mhe. Jaji Kiongozi kuongeza idadi
ya Majaji katika Mahakama kuu Divisheni ya kazi ili mashauri yamalizike kwa
haraka.
Naye
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania-TUCTA, Dkt. Yahaya
Msigwa amesema jamii ina uelewa mdogo wa sheria mbalimbali zinazohusu masuala
ya kazi pamoja na haki za msingi za wafanyakazi hivyo amewaomba wanasheria
kusaidia kuwaelimisha wananchi ili wafahamu haki zao za msingi.
Alisema
endepo wananchi watakuwa na uelewa wa kutosha juu ya sheria hizi itasaidia kupunguza
migogoro ya kikazi isiyokuwa ya lazima.
“Katika
zama hizi maandamano na migogoro ya kikazi haina tija kwa pande zote mbili yaani
kwa watumishi na kwa serikali pia, hivyo ni muhimu wafanyakazi wakazifahamu
vizuri sharia za kazi”, alisema Dkt. Msigwa.
Aidha,
Dkt. Msigwa amewataka waajiri mbalimbali nchini kuhakikishga wanakaa vikao
muhimu na wafanyakazi wao ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima makazini.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi na wadau wanaohusika na utatuzi wa Migogoro ya Kazi wakiwa kwenye Kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya Maandalizi ya Kikao cha Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na Wadau wanaohusika na utatuzi wa Migogoro ya Kazi. Wa tatu Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa Alex na wa tatu kushoto ni Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi Mhe. Lilian Mashaka.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Mahakama Wa tatu Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa Alex na wa tatu kushoto ni Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi Mhe. Lilian Mashaka.
Wajumbe wa kikao cha wadau wakiwa kwenye kikao hicho leo jijini Dar es salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akiwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa Alex kwenye kikao hicho.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wasajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania mara baada ya kufungua kikao cha Wadau.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni