Na
Mary Gwera
KAMA ilivyo kwa huduma
nyingine katika jamii, huduma ya upatikanaji wa HAKI ni miongoni mwa huduma ambazo wananchi wanahitaji kwa wakati
bila longolongo, kufuatia uhitaji huu wa Wananchi, Mahakama ya Tanzania imekuwa na inaendelea
katika jitihada za kuboresha huduma ya upatikanaji wa haki kwa kujenga na
kukarabati miundombinu bora na wezeshi ya kutolea haki.
Tukiangazia Mkoa wa
Mara ambapo kwa kipindi kirefu wananchi wake wamekuwa na wanaendelea kupata
shida hususani katika upatikanaji wa huduma ya haki kwa ngazi ya Mahakama Kuu
ambapo Mwananchi mwenye kesi anatakiwa kusafiri kwa kilomita zipatazo 218 kwenda
Mahakama Kuu Mwanza ili kutafuta haki yake.
Kulingana na uhitaji mkubwa
wa huduma ya Haki nchini, Mahakama ya
Tanzania imekuwa ikifanya ujenzi na matengenezo ya majengo yake kwa awamu
kulingana na hali ya bajeti, kwa sasa Mahakama ya Tanzania imeanza ujenzi wa
Mahakama Kuu katika mikoa miwili ambayo ni Mara na Kigoma.
Katika mahojiano maalum
na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Bibi. Zilliper Geke
yaliyofanyika ofisini kwake Mahakama ya Mkoa-Musoma, Februari 13, Bi. Zilliper anasema
kuwa ujenzi wa Mahakama Kuu unaoendelea katika Kanda hiyo umeleta faraja na ukombozi
mkubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Mara kwani wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu
kusafiri kilometa kadhaa kwenda mkoani Mwanza kutafuta haki zao kwa ngazi ya
Mahakama Kuu.
“Kwakweli wananchi wa
Mkoa huu na hata wateja wanaokuja katika Mahakama ya Mkoa, wanaonekana
kufurahia ujenzi wa Mahakama Kuu Musoma ambapo pindi itakapokamilika
itawaondolea usumbufu wa kusafiri hadi Mwanza kupata huduma” alieleza Mtendaji
huyo.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Kampuni ya D.F MISTRY& CO (1974) LTD, Kampuni ambayo imepata
tenda ya ujenzi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Musoma, Eng. Bhavesh anasema ujenzi wa
Mahakama hiyo ulioanza rasmi Novemba 11, 2017 unaendelea vizuri kama ratiba ilivyopangwa.
“Ujenzi wa Mahakama Kuu
Musoma umepangwa kumalizika ndani ya miezi 18 ambao ni sawasawa na mwaka mmoja
na nusu, hivyo kwa hatua tuliyofikia sasa tuko mbele zaidi hali ambayo inaridhisha
kuwa ujenzi huu tutamaliza ndani ya muda kama hakutakuwa na changamoto yoyote,”
alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha Eng. Bhavesh anabainisha
juu ya hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa sasa kuwa ni ujenzi wa ghorofa ya kwanza
‘first floor’ ya jengo hilo ambayo anasema kuwa itachukua muda wa takribani
mwezi mmoja hadi kukamilika kwa hatua hiyo.
“Hatua hii ya ujenzi
itatuchukua takribani mwezi mmoja toka sasa, kwa sasa tunakwenda vizuri, hivyo
mara baada ya kukamilika kwa hatua ya ujenzi ya ghorofa ya kwanza tutaendelea
na ghorofa ya pili, na kazi hii ya ujenzi wa jengo zima la Mahakama Kuu Musoma
inatakiwa kukamilika ifikapo Aprili 19, 2019,” alieleza Eng. Bhavesh.
Akionyesha kufurahishwa
na ujenzi wa Mahakama hiyo, kwa upande
wake Wakili wa Kujitegemea-Mkoani Mara, Bw. Thomas Makongo anaeleza kuwa uamuzi
wa Mahakama ya Tanzania kujenga Mahakama Kuu-Musoma utasaidia kuharakisha ‘speed
up’ mashauri na kuipunguzia mlundikano wa Mashauri Mahakama Kuu-Kanda ya
Mwanza.
“Hata hivyo naweza
kusema kuwa, ujenzi wa Mahakama Kuu Mara umechelewa sana kwa sababu mkoa huu
una mashauri mengi ya Jinai hususani ya mashauri ya Mauaji, kwahiyo kukosekana
kwa Mahakama Kuu katika Mkoa huu kumechangia ucheleweshaji wa mashauri haya
kusikilizwa na kumalizwa kwa wakati,” alisema Wakili Makongo.
Aidha, Wakili huyo
anaendelea kusema kuwa kuwepo kwa Mahakama Kuu Mara kutasaidia pia kushughulikia
migogoro dhidi ya Watendaji wa Mahakama kwa ukaribu zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa
Kitengo cha Ujenzi, Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi amesema kuwa
ujenzi wa Mahakama Kuu Musoma ambao unasimamiwa na ‘HAB Consult’ na ‘Mbega Associates’
unaenda sambasamba na Ujenzi wa Mahakama Kuu Kigoma.
“Kukamilika kwa
Mahakama Kuu hizi mbili kutafanya idadi ya kuwa na jumla ya Kanda za Mahakama
Kuu 16 kati ya mikoa 26, na hivyo uhitaji utakaobaki ni wa Majengo 10 tu,”
alieleza Mhandisi Kitunzi.
Hata hivyo, Mhandisi
Kitunzi anasema kuwa taratibu za ujenzi wa Mahakama Kuu katika baadhi ya mikoa
iliyobaki zinaendelea, na Mahakama hizo zitajengwa chini ya Fedha za Mradi wa
Benki ya Dunia (WB) Mikoa itakayojengewa Mahakama Kuu/Vituo vya Haki ‘Justice
centre’ ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Singida, Mwanza na
Arusha.
Aidha; kwa upande wa
ujenzi wa Mahakama za Hakimu Mkazi, Mhandisi Kitunzi anabainisha kuwa ujenzi wa
Mahakama hizo pia unaendelea katika mikoa ya Geita, Njombe, Lindi, Katavi na
Simiyu.
Azma ya Mahakama ya Tanzania ni kusambaza
huduma za Mahakama nchi nzima ili hata mwananchi aliyepo katika ngazi ya Kata
aweze kupata huduma ya Haki.
Mbali na ujenzi pia
kumekuwa na ukarabati wa majengo ya Mahakama ya mara kwa mar azote zikiwa ni
jitihada za kuhakikisha kunakuwa na miundombinu ya majengo bora ya kutolea
haki.
Hivi karibuni katika
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria na Siku ya Sheria nchini jumla ya Majengo mapya
matano (5) ya Mahakama yalizinduliwa rasmi; majengo hayo ni pamoja na Kituo cha Mafunzo na Habari za Mahakama
kilichopo Kisutu Dar es Salaam, Mahakama
ya Wilaya Bagamoyo, Mahakama ya
Wilaya Kigamboni, Mahakama ya Wilaya
Mkuranga pamoja na Mahakama ya
Mwanzo Kawe.
Mmoja wa Wahandisi
kutoka Kampuni ya D.F MISTRY& CO (1974) LTD, inayojenga jengo la Mahakama
Kuu Musoma akionyesha mchoro wa jengo hilo la Mahakama linalojengwa.
Muonekano
wa mbele ya jengo hilo .
Mafundi wakiendelea na ujenzi.
Wahandisi wa Mradi huo wakitoa maelezo ya hatua ya ujenzi waliyofikia kwa sasa.
Muonekano wa sehemu ya jengo la Mahakama Kuu-Musoma likiendelea kujengwa.
Muonekano wa upande wa kulia wa jengo hilo.
wa ghorofa ya kwanza ya jengo hilo litakalokuwa na ghorofa mbili.
Mafundi wakiendelea na ujenzi.
Wahandisi wa Mradi huo wakitoa maelezo ya hatua ya ujenzi waliyofikia kwa sasa.
Muonekano wa sehemu ya jengo la Mahakama Kuu-Musoma likiendelea kujengwa.
Muonekano wa upande wa kulia wa jengo hilo.
wa ghorofa ya kwanza ya jengo hilo litakalokuwa na ghorofa mbili.
Muonekano
wa ghorofa ya kwanza ‘first floor’ ya jengo hilo: Mafundi wakiendelea kujenga.
Mtendaji-Mahakama ya
Hakimu Mkazi-Musoma, Bi. Zilliper Geke akiongea jambo katika mahojiano maalum.
Wakili wa Kujitegemea-Mkoani Mara, Bw. Thomas Makongo akiwa katika sura ya furaha pindi alipokuwa akitoa maoni yake kufuatia ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, katika maongezi yake Wakili huyu ameonyesha kufurahishwa na hatua hii ya ujenzi akisema kuwa upatikanaji wa Mahakama hii utasaidia kupunguza mlundikano wa Mashauri Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza na vilevile kuwapunguzia aza ya kusafiri kilomita kadhaa kutafuta haki.
(Picha na Mary Gwera, Musoma-Mara)
Wakili wa Kujitegemea-Mkoani Mara, Bw. Thomas Makongo akiwa katika sura ya furaha pindi alipokuwa akitoa maoni yake kufuatia ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, katika maongezi yake Wakili huyu ameonyesha kufurahishwa na hatua hii ya ujenzi akisema kuwa upatikanaji wa Mahakama hii utasaidia kupunguza mlundikano wa Mashauri Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza na vilevile kuwapunguzia aza ya kusafiri kilomita kadhaa kutafuta haki.
(Picha na Mary Gwera, Musoma-Mara)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni