VIKAO
VYA MAHAKAMA YA RUFANI VYAANZA RASMI MBEYA WAZINDUA KWA GWARIDE MAALUM.
Vikao vya Mahakama ya
Rufani vimeanza kusikilizwa leo Mahakama Kuu Mbeya, vikao hivyo vitakavyodumu
kwa muda wa mwezi mmoja vimezinduliwa kwa gwaride maalum lililofanyika katika
Viwanja vya Mahakama Kuu Mbeya ambapo Mwenyekiti wa Jopo hili ni Mhe. Jaji
Benard Luanda, Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye amelikagua
Wahe. Majaji wengine wa
Mahakama ya Rufani waliopo katika jopo hilo ni Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika na
Mhe. Jaji Bethuel Mmila, katika vikao
hivyo vya mwezi mmoj, jumla ya Mashauri
27 yatasikilizwa huku Mashauri 19 yakiwa ya Jinai na Mashauri nane (8) yakiwa
ya Madai.
Jaji wa Mahakama ya
Rufani (T), Mhe. Benard Luanda akikagua gwaride maalum katika Viwanja vya
Mahakama Kuu-Mbeya kuashiria uzinduzi rasmi wa vikao cha Mahakama ya Rufani
vilivyoanza rasmi Februari 05, 2018.
(Picha na Rajabu
Singana, Mahakama Kuu-Mbeya)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni