Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe. Firmin Matogolo amewataka Watumishi wa Divisheni hiyo kufanya kazi kwa kufuata Maadili ili kujenga taswira chanya ya Mahakama ya Tanzania kwa wananchi.
Akifungua kikao kazi
cha Watumishi wa Mahakama hiyo ambacho pia kilijumuisha Mafunzo kuhusu Mpango Mkakati wa miaka Mitano wa Mahakama ya
Tanzania (2015/16 -2019/20) kwa
watumishi hao, Jaji Matogolo aliwataka watumishi kuzingatia suala la maadili na
kulipa kipaumbele kama ambavyo jamii inatarajia kutokana na umuhimu wa
Divisheni hiyo.
“Kuweni makini
mnapotekeleza majukumu yenu kutokana na umuhimu wa Divisheni ya Makosa ya
Rushwa na Uhujumu Uchumi kwani Serikali pamoja na Wananchi wametuamini sisi,
alisema”
Jaji Matogolo pia aliwaasa
watumishi wa Mahakama hiyo kujifunza kwa bidii na kuufahamu Mpango Mkakati wa
Mahakama ili waweze kuutekeleza ipasavyo na kuboresha huduma wanazotoa kwa
wananchi.
Alisema pamoja na
changamoto zinazoikabili Divisheni hiyo mpya za upungufu wa watumishi, Jaji
Matogolo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii wakati Mahakama ya
Tanzania ikizitafutia majibu changamoto hizo ambapo alisema Mpango Mkakati wa
Mahakama ya Tanzania unalenga pia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili
watumishi wa Mahakama.
Akiwasilisha Mada juu
ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Bwn. Benjamin Mlimbila pia alisisitiza
suala la Maadili kwa watumishi na kuwataka kuzingatia kipembele katika nguzo ya
Tatu ya Mkakati huo kinachowataka kuimarisha tabia, maadili na miiko ya
watumishi wa Mahakama.
Wakati
huo huo, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe. Charles Magesa pia aliwataka
watumishi hao kutekeleza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa kujituma pamoja na kutii
Mamlaka katika maeneo yao ya kazi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe. Firmin Matogolo akifungua kikao kazi cha Watumishi wa Divisheni hiyo ambacho pia kilihusisha Mafunzo ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/16-2019/20) . Kushoto ni Naibu Msajili wa Divisheni hiyo Mhe. Charles Magesa.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Bwn. Benjamin Mlimbila akizungumza wakati akitoa Mada kuhusu Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/16-2019/20) kwa Watumishi wa Divisheni hiyo.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Bwn. Benjamin Mlimbila akiwa pamoja na Watumishi wa Divisheni hiyo wakati wa kikao kazi leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe. Charles Magesa akizungumza na watumishi wa Mahakama hiyo (hawapo Pichani) leo jijini Dar es salaam |
Msaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Nathanael Malela akizungumza wakati wa kikao kazi ambacho pia kilihusisha Mafunzo ya Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Watumishi wa Divisheni hiyo.
Mhasibu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Bibi Joyce Mulugu akisoma Taarifa ya Makisio ya Bajeti ya Divisheni hiyo wakati wa kikao kazi cha watumishi hao.
Baadhi ya Watumishi wa Divisheni hiyo wakifuatilia jambo wakati wa kikao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni