Jumatano, 28 Machi 2018

MAFUNZO YA WAHE. MAJAJI YAMALIZIKA-ARUSHA



Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi akitoa hotuba ya kufunga Mafunzo wa siku tano ya Waheshimiwa Majaji yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha, kushoto ni Mhe. Sophia Wambura, Jaji wa Mahakama Kuu-Kitengo cha Ardhi.

Waheshimiwa Majaji wakimsikiliza mgeni rasmi alipokuwa akifunga mafunzo yao rasmi.

Mhe. Sophia Wambura, Jaji wa Mahakama Kuu-Kitengo cha Ardhi akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi aliyefunga mafunzo hayo.

Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Tabora, Mhe. John Utamwa akipokea cheti cha ushiriki wa Mafunzo kutoka kwa  Kaimu Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi.
Mhe. Haruna Songoro, Jaji wa Mahakama Kuu-Divisheni ya Biashara akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mgeni rasmi.
Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza, Mhe. Joaquine De Mello akipokea cheti cha ushiriki wa Mafunzo.



Mhe. Latifa Mansoor, Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Dodoma akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi.
Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Mhe. Modesta Makopolo Opiyo akipokea cheti cha ushiriki, katika Mafunzo hayo Wahe. Majaji wametakiwa kuzingatia na kutekeleza yale yote waliyofunzwa ili kuboresha zaidi huduma ya utoaji haki nchini.
(Picha na Mary Gwera)


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni