Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Juma akifungua kikao cha Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya
Rufani, lengo la kikao hicho cha siku moja kimelenga katika kufanya tathmini
yaUtendaji kazi wa Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2017 na kuweka Mkakati na malengo
ya mwaka, 2018, kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Benard Luanda.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao hicho akiendesha
kikao cha Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, kushoto ni Jaji namba moja wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jaji Mbarouk S. Mbarouk, kulia
ni Mhe. Jaji Benard Luanda.
Sehemu ya Waheshimiwa
Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika hicho kilichofanyika katika Ukumbi
wa Hoteli ya ‘Oceanic’ iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya Waheshimiwa
Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na
Wasaidizi wa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika kikao
hicho.
Waheshimiwa Majaji
wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu wakati akitoa neno la ufunguzi.
Msajili Mkuu, Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati akitoa Mada ya Mpango Mkakati wa Mahakama
kwa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani waliopo katika kikao cha tathmini
na uwekaji wa mpango wa malengo ya utekelezaji kwa mwaka huu.
Msajili-Mahakama ya
Rufani (T) akitoa Mada katika Kikao cha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani (T),
katika Mada yake Mhe. Msajili amesema kuwa Mahakama ya Rufani imefanikiwa
kushusha kiwango cha mlundikano kutoka asilimia 37 mwaka 2016 hadi asilimia 10
mwishoni mwa Desemba, 2017, vilevile kwa mwaka huu 2018, Mahakama ya Rufani imejipanga Kusikiliza Mashauri na Kuimarisha Masjala.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Juma (katikati) pamoja na Majaji wengine wa Mahakama ya
Rufani Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Wasajili ya Mahakama
ya Rufani.
Picha ya pamoja: Mhe.
Jaji Mkuu, Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Wasajili wa Mahakama ya
Rufani na Wasaidizi wa Sheria wa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
(Picha na Mary
Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni