Na
Sheiba Bulu, Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri wa Katiba na
Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu
mkoani Mara na kujionea ujenzi huo unavyoendelea .
Akizungumza baada ya
kupata taarifa fupi kuhusu ujenzi wa Mahakama hiyo mapema Machi 20, 2018, Prof.
Kabudi amewataka Wasimamizi wa Mradi huo kuutangaza kwani uwepo wa Mahakama Kuu Mkoani Mara utaleta ahueni kubwa
kwa wananchi wa mkoa huo ambao walikuwa wanalazimika kwenda Mwanza kutafuta
haki zao.
Mhe. Waziri amesema
Mahakama hiyo itakapokamilika wananchi wa mkoa wa Mara watapata haki zao kwa
wakati ndani ya mkoa wao bila ya kulazimika kwenda umbali mrefu kutafuta haki.
Ujenzi wa Mahakama Kuu
mkoani Mara unatekelezwa kupitia Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama wa
2015/2016-2019/2020 ambao unatoa kipaumbele kwa ujenzi wa miuundombinu ya
Mahakama nchini ili kusogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi.
Waziri wa Katiba wa
Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, akisaini kitabu cha Wageni pindi
alipowasili eneo la Mradi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu lililopo Bweri Manispaa ya
Musoma.
Mtendaji wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Musoma, Bi. Zilliper Geke akisoma taarifa ya maendeleo ya Mradi mbele ya Mhe. Waziri
Prof. Palamagamba Kabudi.
Mhe. Waziri akielekea
kukagua jengo la Mahakama Kuu-Kanda ya Musoma linaloendelea kujengwa na Kampuni
ya Ujenzi ya ‘DF-MISTRY COMPANY LTD’
Mafundi wakiendelea na
kazi.
Mhe. Waziri akiwa na
Makarandasi wanaojenga jengo hilo pindi alipokuwa anakagua.
Ukaguzi ukiendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni