Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akifungua Kikao cha Wadau
Kujadili kazi ya ulinganisho wa chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) na
Vyuo vingine vya Mafunzo endelevu. Kikao hicho kati ya Chuo cha Uongozi wa
Mahakama na Wadau wa Vyuo vingine vinavyotoa mafunzo endelevu kimelenga katika
kujadili uzoefu na nafasi ya ushirikiano wa karibu baina ya Chuo hicho na Vyuo
vingine vya Umma vinavyotoa mafunzo endelevu kwa Watumishi wa umma na Wadau
mbalimbali katika Sekta ya Sheria, kikao
hicho kilifanyika Aprili 16 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwl. Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji
Mstaafu, Mhe. John Mrosso akiongea jambo na Wadau walioshiriki katika kikao
hicho, katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, kushoto ni
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.
Wajumbe
wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, alipokuwa akielezea kuhusu Chuo hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa
Kikao walioshiriki ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha
Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora,Chuo
cha Kodi n.k, aliyeketi nyuma wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila.
Wajumbe wa
Kikao walioshiriki ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha
Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora,Chuo
cha Kodi n.k, Washiriki wakifuatilia kwa makini,
katika kikao hicho Chuo cha Uongozi wa Mahakama kwa kushirikiana na Mahakama ya
Tanzania wamechukua maoni yote yaliyotolewa na Wadau hao na wameahidi kuyafanyia
kazi katika kuboresha Mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho kwa manufaa ya
Watumishi wa Mahakama na Wananchi kwa ujumla.
Picha ya
pamoja ya ushiriki: aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.
Ibrahim Hamis Juma, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu,
Mhe. John Mrosso, wa pili kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila, wa
kwanza kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali
na wa kwanza kushoto ni Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo, Mkuu wa Chuo cha Uongozi
wa Mahakama-Lushoto (IJA).
(Picha
na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni