Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Makaramba (wa tatu kulia), pamoja
na Viongozi weengine wa Mahakama katika Kanda hiyo wakiwa katika picha ya
pamoja na sehemu ya Watumishi waliohudhuria katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi
wa Mahakama Kanda ya Mwanza, kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa JS ‘Motel’
uliopo wilayani Chato.
Jaji
Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya Watumishi walioshiriki katika kikao hicho, walioshiriki ni pamoja
na Mtendaji, Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza, Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza, Wajumbe wa Baraza, pamoja na Maafisa Utumishi na Tawala wote wa Kanda
ya Mwanza, katika kikao hicho Mhe. Jaji Mfawidhi amewataka Watumishi wa Kanda
hiyo kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama, kuzingatia
nidhamu na maadili katika kazi, na utoaji huduma kwa wateja unaotoa matokeo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni