Na
Lydia Churi, Magreth Kinabo-Mahakama
Akizungumza na
Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Jaji Mkuu amesema TLS ni chama
huru cha kitaaluma kwa kuwa kilianzishwa kwa mujibu wa sheria kufanya kazi kwa manufaa
mapana ya Umma.
“Hatuwezi kukubali chama hiki kikajisemea kuwa wao ni chama binafsi na tukakubali, dhana ya ubinafsi haipo”, alisisitiza Jaji Mkuu.
“Hatuwezi kukubali chama hiki kikajisemea kuwa wao ni chama binafsi na tukakubali, dhana ya ubinafsi haipo”, alisisitiza Jaji Mkuu.
Alisema
jukumu la TLS ni Kuisaidia Serikali na Mahakama kuhusu mambo yoyote yanayogusa
sheria, utawala wa sheria na kazi za kisheria na akaongeza kuwa dhana hii ndiyo
inayoiunganisha Taasisi hiyo na Mahakama ya Tanzania.
Jaji Mkuu pia
amewashauri viongozi wa chama hicho kumuheshimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kwa kuwa Sheria na Kanuni zote ni lazima zipitie kwake.
Alisema
Mamlaka ya Baraza la Uongozi la TLS katika Kutekeleza Majukumu ya Umma ni kusaidia
kuboresha elimu ya sheria na taaluma ya Sheria Tanzania na kuwawezesha
wanataaluma wa sheria kupata elimu ya ziada ya sheria kwa kadri mabadiliko
yanayotokea nchini na duniani.
TLS
ni Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria za nchi kabla ya Uhuru na
kukubalika kuendelea kuwepo kama Taasisi ya Kisheria kwa malengo ya kuanzishwa
kwake kuelekezwa kwenye manufaa ya umma kwa kushirikiana na Mahakama, Bunge, pamoja
na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akizungumza na waandishi wa habari alipokutana
nao leo. Katika Mkutano huo Mhe. Jaji Mkuu amekitaka Chama cha Mawakili
Tanganyika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria kwani ni Taasisi ya Umma na si Chama binafsi, kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali,
na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw.
Hussein Kattanga.
Mhe. Jaji Mkuu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Sehemu ya waandishi wa
habari wakiwa katika Mkutano huo.
(Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni