Jumatano, 20 Juni 2018

BENKI YA DUNIA YAKAGUA BAADHI YA MIRADI YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MAHAKAMA

  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kigamboni Mhe. Sundi Benneth Fimbo akiwatembeza wageni kutoka Benki ya Dunia ili kuliona jengo jipya la Mahakama ya Wilaya  na Mwanzo ya Kigamboni lililojengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia. Nyuma ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik na kushoto ni Mshauri wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya Kazakhstan, Bi. Nazgul Yergaliyeva 
 Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik akiwaelezea jambo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kigamboni Mhe. Sundi Benneth Fimbo pamoja na Mshauri wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya Kazakhstan, Bi. Nazgul Yergaliyeva walipotembelea Mahakama hiyo jijini Dar es salaam.
 Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik akiwaelezea jambo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kigamboni Mhe. Sundi Benneth Fimbo pamoja na Mshauri wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya Kazakhstan, Bi. Nazgul Yergaliyeva walipotembelea Mahakama hiyo jijini Dar es salaam.
 Wananchi wakiwa katika Mahakama ya Wilaya na Mwanzo ya Kigamboni wakisubiri huduma.
 Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama Mhe. Zahara Maruma akijadiliana jambo na Mtaalamu wa Benki ya Dunia Bi. Clara Naghani, wataalamu hao walipotembelea Mahakama ya wilaya na Mwanzo ya  Kigamboni.
 Wataalamu kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik (kushoto), Clara Maghani (kulia) pamoja na Mshauri wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya Kazakhstan, Bi. Nazgul Yergaliyeva wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kigamboni Mhe. Sundi Benneth Fimbo na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania Mhe. Zahara Maruma walipotembelea Mahakama hiyo jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania Mhe. Zahara Maruma akiwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya na Mwanzo ya Kigamboni Mhe. Sundi Benneth Fimbo
  Wataalamu kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik (kushoto), Clara Maghani (kulia) pamoja na Mshauri wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya Kazakhstan, Bi. Nazgul Yergaliyeva (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wao Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania Mhe. Zahara Maruma walipotembelea Kituo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es salaam.
 Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ilvin Mugeta akielezea jambo kwa Wataalamu kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik na Clara Maghani (hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa katika kuandaa Mfumo wa Upelelezi na Uendashaji wa Mashauri. Mahakama ya Tanzania katika hatua yake ya Kuboresha Huduma, inaandaa Mfumo huu ili Haki iweze kupatikana kwa wakati.

Bw. Laurean Tibasana ambaye ni Facilitator wa Kamati ya kuandaa Mfumo wa Upelelezi na Uendashaji wa Mashauri akizungumza jambo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni