Pichani ni Jaji wa
Mahakama Kuu ya Uganda, Mhe. Paul Gadenya akitia saini kitabu cha wageni pindi
alipowasili katika Mahakama ya Wilaya Kigamboni kujionea jengo hilo la kisasa
lililojengwa kwa teknolojia ya ujenzi ya Moladi, mbali na kutembelea jengo
hilo Jaji Gadenya ametembelea pia Ofisi za Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ‘JDU’
kupata taarifa ya maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ndani ya
Mahakama kwa lengo la kuboresha huduma za utoaji haki nchini, aliyesimama kulia
ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi
wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo, akimpitisha Mhe. Jaji
Gadenya kukagua sehemu mbalimbali za jengo hilo la kisasa, aliyepo nyuma ya
Mhe. Gadenya ni Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Tathmini, Mahakama, Bw.
Sebastian Lacha.
Mhe. Jaji Gadenya (kushoto)
akijadili jambo na wenzake, kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya
Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na
Tathmini, Mahakama, Bw. Sebastian Lacha.
Picha ya pamoja nje ya
jengo jipya la kisasa la Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni,
Mhe. Gadenya ameisifu Mahakama kwa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika
na ambayo tayari ameshafanyika kwa ustawi wa Wananchi.
(Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni