Jumatatu, 2 Julai 2018

WANANCHI WAENDELEA KUMIMINIKA KWENYE BANDA LA MAHAKAMA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI


Mtumishi wa Mahakama (mwenye fulana nyekundu) akimkaribisha mwananchi kwenye banda la Mahakama lililopo katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa.

Mwananchi akijiandikisha katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mahakama.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanaoshiriki katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa.
Mwananchi akiwasilisha malalamiko yake kwenye sehemu ya Malalamiko iliyo ndani ya Banda la Mahakama ya Tanzania.
Naibu Msajili, Mhe. Charles Magesa akiwafafanulia wananchi jinsi Mfumo wa Usajili wa Mawakili unavyofanya kazi.
Mwananchi akiingia katika banda la Mahakama kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.
 Maofisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakitoa maelezo mbalimbali kwa wananchi waliotembelea sehemu hiyo iliyopo ndani ya banda la Mahakama.
Wananchi waliojitokeza kupata msaada wa kisheria kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika iliyomo ndani ya banda la Mahakama.
Mfawidhi wa Kitengo cha Mirathi-Mahakama, Bw. Cassian Makene (kulia) akiwafafanulia wananchi kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo Mirathi.
Mfano wa gari litakalotumika kama Mahakama inayotembea (mobile court) ili kusogeza huduma ya utoaji haki kwa wananchi. Gari hili linapatikana mbele ya banda la Mahakama ya Tanzania kwenye Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa.
 

 
 
 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni