Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga pamoja na Shirika la Posta nchini wameendelea kusafirisha nyaraka za kimahakama kupitia Huduma ya Posta Mlangoni ambapo hivi sasa nyaraka hizo hufikishwa kwa wakati kwa wadau na wateja wa mahakama popote walipo.
Akitoa Elimu ya namna nyaraka za kimahakama zinavyoweza kuwafikia wateja na wadau wa Mahakama, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga Bw. Ernest Masanja amesema kwa sasa wananchi hao hawana tena haja ya kusafiri umbali mrefu kufuatilia nyaraka mbalimbali ikiwemo nakala za hukumu na mwenendo wa mashauri.
“Huduma hizo zitawafikia
nyumbani na Afisa wa Shirika la Posta ambaye amepewa jukumu la kusambaza
nyaraka hizo atawagfikishia”, alisema Mtendaji huyo alipokuwa akiwaelimisha
wananchi waliofika Mahakamani hapo kupata huduma.
Kwa upande wao,
wananchi na wadau wa Mahakama wamefurahia huduma hiyo kwani wamesema itawasaidia
kuondoa gharama pamoja na kupunguza usumbufu wa kusafiri kutoka umbali mrefu kwa
ajili ya kufuatilia nakala za hukumu pamoja na mwenendo wa Mashauri.
Mwezi Aprili mwaka
2018, Mahakama ya Tanzania na Shirika la Posta nchini walisaini Mkataba ambapo
shirika hilo litakuwa likisafirisha na kusambaza nyaraka mbalimbali za
kimahakama kwa wateja wa Mahakama zikiwemo nakala za hukumu, mwenendo wa kesi
pamoja na nyaraka nyinginezo.
Mtendaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Bw. Ernest Masanja akifafanua jambo kwa wateja wa Mahakama kuhusu Huduma ya Posta Mlangoni.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Bw. Ernest Masanja akifafanua jambo kwa wateja wa Mahakama kuhusu Huduma ya
Afisa wa Shirika la Posta Bw.Silas Nyorobi akiwa tayari kwa ajili ya kusambaza nyaraka za Kimahakama mkoani Shinyanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni