Na Victor
Kitauka, Mahakama ya Mkoa Morogoro
Jaji
Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.Eliezer Feleshi amewataka Watumishi
wa Mahakama ya Mkoa Morogoro kufanya kazi kwa umoja, bidii, ushirikiano na
kupendana kwani wanatumia muda wao mwingi wakiwa kazini.
Jaji
Kiongozi aliwakumbusha watumishi wa Mahakama hiyo alipotembelea Mahakama ya
Mkoa huo kujionea hali ya utoaji haki huku akisisitiza kuwa jukumu kuu la Mahakama
ni kutoa haki kwa kwa wakati hivyo amewata kuwahudumia wananchi kwa
weledi na bidii ili kuondoa malalamiko ya wananchi dhidi ya
mahakama.
Mnamo
tarehe 16/8/2018, Mhe. Jaji Kiongozi alifanya ziara katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Morogoro na kuongea na Watumishi wa Mahakama hiyo.
Awali,
Mh Jaji Kiongozi kabla ya kukutana na kuongea na watumishi wa mahakama
alipata wasaa wa kutembelea kiwanja cha Mahakama kilichopo eneo la Kihonda na
kujionea eneo ambalo linatarajiwa kujengwa jengo la Mahakama Kuu Morogoro
ambapo aliridhishwa na ukubwa wa kiwanja hicho na eneo kilipo kiwanja
hicho.
Aidha
Mhe.Jaji Kiongozi aliwaonya watumishi wazembe kazini na
wanaojiusisha na vitendo vya rushwa kuwa Mahakama haitomvumilia Mtumishi
yeyote mzembe na anayejihusisha na vitendo vya rushwa
Vilevile
Mhe. Jaji Kiongozi, aliwataka Hakimu Mkazi Mfawidhi na Mtendaji wa
mahakama hiyo kutosita kutoa taarifa na kuwachukulia hatua watumishi wote
wazembe na wanaojiusisha na vitendo vya rushwa na itakapogundulika kuwa
viongozi wameshindwa kuwachukulia hatua watumishi basi uongozi wa
mahakama hautosita kuwachukulia hatua viongozi hao kwa kushindwa kuchukua
hatua dhidi ya watumishi wa chini yao ambao ni wazembe na wala
rushwa kwani wanachafua taswira ya Taasisi.
Kabla
ya kumkaribisha Jaji Kiongozi kuongea na watumishi, Hakimu Mkazi Mwandamizi
Mfawidhi, Mh.Elizabeth J.Nyembele alielezea kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Morogoro imefanikiwa mpaka sasa kusikiliza na kutolea maamuzi zaidi ya
asilimia 75 ya mashauri yote yaliyopo mahakamani hapo.
Kwa
upande wa changamoto zinazoikabili Mahakama Hakimu Mkazi
Mfawidhi alimueleza Jaji kiongozi kuwa upelelezi hasa katika kesi za
uhujumu uchumi,kutokufanyika kwa vikao vya mahakama kuu Morogoro kwa siku
za hivi karibuni imeipelekea msongamano wa mahabusu katika gereza
la mahabusu mkoa wa morogoro na uhaba wa watumishi katika kada tofauti
jambo linalopolekea kupunguza ufanisi katika utendaji wa kazi.
Mwisho,
Jaji Kiongozi Mh Jaji dkt Feleshi aliwataka Hakimu Mkazi Mfawidhi na Mtendaji
wa Mahakama ya Morogoro kuendelea kufanya kazi kwa uwazi, ukaribu na
kuwashirikisha watumishi wa chini ili kuondoa malalamiko na kero za watumishi
na aliwaagiza kushughulikia kero na malalamiko ya watumishi zilizo ndani ya
uwezo wao na zile ambazo zipo nje ya uwezo wao waziwasilishe ngazi za juu kwa
utekelezaji.
Jaji
Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.Eliezer Feleshi, akiongea na Watumishi wa Mahakama (hawapo pichani), kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, Mhe. Elizabeth Nyembele na kulia ni Mtendaji Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Bw. Nestory Mujunangoma.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Mkoa, Morogoro wakimsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, Mhe. Elizabeth Nyembele(kushoto) akimueleza jambo Mhe. Jaji Kiongozi wakati alipotembelea Mahakama ya Mkoa Morogoro.
Mtendaji Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Bw. Nestory Mujunangoma (kushoto) akimueleza jambo Mhe. Jaji Kiongozi.
(Picha na Victor
Kitauka)
Heko mahakama ya morogoro, jitihada zenu zinaonekana, hasa katika utoaji wa haki kwa wakati(umalizaji wa mashauri kwa wakat) hakika wananch tunaridhishwa na utendaji kazi wenu!! Uanzishwaji wa mahakama ya wilaya ya mvomero ambayo hapo awali haikuwepo ni ishara tosha kua mmedhamiria kuwafikisha wananchi huduma zenu kwa karibu!
JibuFutaNa mbonde wa mbonde
Futa