Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Sam M. Rumanyika akizindua zoezi
la utoaji wa elimu kwa umma katika Viwanja vya Mahakama Kuu Mwanza. Zoezi hilo
lilifanyika mwishoni mwa wiki kuanzia saa 2:30 - 3:00 asubuhi kwa ngazi zote za
Mahakama za Kanda ya Mwanza ( Mwanza, Mara na Geita).
Aidha
uzinduzi umeambatana na kampeni ya Kanda ambayo ni "MPE RAHA MTEJA
MAHAKAMA ING'ARE" na mada iliyotolewa ni Haki na Masharti ya Dhamana.
Zoezi hili ni endelevu na litakuwa linafanyika kila siku ya Alhamisi saa 2:30 -
3:00 asubuhi kwa Mahakama zote za Kanda ya Mwanza.
Wananchi
wakimsikiliza Mhe. Jaji Mfawidhi (hayupo pichani).
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Mwanza, Mhe. Rhoda Ngimilanga akitoa
elimu kwa wananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni