Na Festo Sanga, Mahakama ya Mkoa-Kigoma
Mahakama
ya Hakimu mkazi Kigoma imeendelea kuratibu vikao vya mashauriano na wadau (case
flow management) kwa kuwashirikisha katika shughuli za uondoshaji wa mashauri ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa
mahakama(2015/16-2019/20) nguzo ya pili
Unaolenga kuwezesha upatikanaji na utoaji wa haki kwa wakati.
Akifungua
kikao hicho kilichoketi mwishoni mwa wiki Agosti 17, 2018, Hakimu Mkazi Mfawidhi
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Mhe. Flora Mtarania ambaye ni mwenyekiti wa
kikao hicho alisisitiza kuwa Vikao hivi vinasaidia kwa kiasi kikubwa kuchambua
na kubaini changamoto mbalimbali.
“Vikao
hivi vinasaidia kwa pamoja kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto husika
na hivyo kuongeza kasi ya uondoshaji wa mashauri kuelekea lengo la sifuri tatu (zero
case, zero backlog na zero complaints),” alisema Mhe. Mtarania.
Aidha
amesisitiza kuwa, wadau wa Mahakama wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano ili
kuwezesha matokeo chanya ya utekelezaji wa Mpango Mkakati.
Hata
hivyo wajumbe waliohudhuria kwa pamoja waliazimia kutoa ushirikiano katika
kuhakikisha kuwa shughuli za Mahakama hazikwami.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Mhe. Flora Mtarania (kulia),
akifafanua jambo katika kikao cha kusukuma mashauri.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kibondo, Mhe. Fadhili Mbelwa akichangia
mada katika kikao kilichoketi mapema Agosti 17, 2018.
Wajumbe
wa kikao cha kusukuma mashauri wakifuatilia na kusikiliza moja ya agenda zilizowasilishwa
katika kikao hicho.
Picha
ya pamoja ya wajumbe wa kikao cha kusukuma mashauri mara baada ya kikao
kumalizika.
(Picha
na Festo Sanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni