Na Magreth Kinabo
Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mhe.Profesa Ibrahim Hamis Juma, ameahidi kufanya kazi kwa
ushirikiano na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kuiwezesha kufanya
majukumu ipasavyo.
Kauli hiyo
imetolewa mapema Agosti 23,wakati Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Julius
Mashamba na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali ,Dkt. Ally Possi, akiwemo Mwanasheria
Mwandamizi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo
walipomtembelea Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es
Salaam.
“Kazi yenu
nyingine ni kuzifahamu sheria na kuangalia na kuzifuatilia,”
alisema Jaji Mkuu.
Aliongeza
kwamba Taasisi hii ni muhimu, na itakuwa
inafanya kazi ya kushauri katika masuala yanayohusu sheria, hivyo
itasaidia kuweka nidhamu katika utendaji kazi unaozingatia misingi ya sheria.
Profesa
Juma alisema watumiaji wa sheria ni wengi, hivyo suala la
kurekebisha sheria linahitaji busara.
Awali Wakili
Mkuu huyo wa Serikali, Mashamba alisema aliomba ushirikiano kati ya ofisi yake
na Mahakama ya Tanzania katika Mfumo wa Kuhifadhi Takwimu za
Mashauri kwa njia ya Kielektroniki na mafunzo ili kuweza kusaidia kuimarisha
ofisi hiyo.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Profesa
Ibrahim Hamis Juma (kulia), akizungumza jambo na Wakili Mkuu wa Serikali, Mhe Dkt. Julius Mashamba (katikati)
kushoto ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi.
Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe.Profesa Ibrahim Hamis Juma(kulia),
akimkabidhi Nakala za Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Julius Mashamba(katikati), kushoto ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali ,Dkt. Ally
Possi.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni