Na
Amina Ahmad, Mahakama Kuu-Tanga
Mahakama
Kuu, Kanda ya Tanga imewapongeza baadhi ya Watumishi wake waliofanya vizuri kwa
kuwapa vyeti maalum ikiwa ni ishara ya kutambua mchango pamoja juhudi zao
katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Vyeti
hivyo vilitolewa kwa Watumishi hao Agosti 24, 2018 na Mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa
wa Tanga, Bw. Martine Shigela, katika hafla
fupi ya kuwaaga Wahe. Majaji na Mahakimu waliohamishwa vituo pamoja na
watumishi wa kada mbalimbali waliostaafu.
Utaratibu huu umeanzishwa
katika Kanda hii ili kuenzi jitidaha na ufanisi wa kazi waliokuwa nao kipindi
cha utumishi wao.
Miongoni
mwa Watumishi waliopatiwa vyeti hivyo ni pamoja na Mahakimu wa Mahakama za
Wilaya na Mahakama za Mwanzo, Maafisa Utumishi, Wasaidizi wa Kumbumbuku,
Wahasibu, Makatibu Mahsusi, Madereva, Walinzi, Mahakama za Wilaya zilizofanya
ukarabati mkubwa wa Mahakama za Mwanzo, Kituo kilichoongoza kwa watumishi wake
kuvaa sare na kuonekana nadhifu pamoja na Mahakama za Wilaya na Mwanzo
zilizosikiliza na kuamua mashauri kwa asilimia nyingi kuliko zingize.
Watumishi waliostaafu
ambao waliagwa katika hafla hiyo ni Bwana. Jumbe Athumani Kai, Msaidizi wa hesabu,
Mahakama ya Wilaya Korogwe, Bi. Lydia Yohana Andrew (Msaidizi wa kumbukumbu,
Mahakama ya mwanzo Mashewa Wilayani Korogwe) na Bi. Shehu Ally Muhsin (Msaidizi
wa kumbukumbu, Mahakama ya Wilaya ya Tanga).
Sambasamba na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Viongozi wengine waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na Mkuu wa chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto IJA, Mhe Jaji Faustine Kihwelo, Mkuu wa Wilaya wa Handeni, Mhe.
Godwin Gondwe, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Mhe. Sauda Mtondoo), Mkuu wa Wilaya
ya Korogwe, Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias
Mwilapwa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji - Korogwe (Mhe. Nicodemus John Bee,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mhe. na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Tanga (Benedict Wakulyamba).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Mhe. Martine Shigela akizungumza jambo katika haflla hiyo, wa pili kushoto ni Mhe. Jaji Imani Aboud na kulia ni
Kaimu Jaji Mfawidhi Kanda ya Tanga, Mhe. Edson Mkasimongwa.
Viongozi mbalimbali wa
Serikali mkoani Tanga waliohudhuria katika hafla hiyo.
Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Mhe. Martin Shigela akimkabidhi Jaji Aboud zawadi alikuwa ameandaliwa na Uongozi wa
Mahakama Kuu Tanga.
Baadhi ya watumishi
waastafu walioagwa kwenye hafla hiyo, kushoto ni Bi. Lydia Yohana
Andrew na kulia ni Bi. Shehu Ally Muhsin.
Mhe. Arnold
Kileo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, akipokea cheti
kwa kushika nafasi ya kwanza kwa Mahakimu wa Wilaya walisikiliza na kumaliza
mashauri mengi.
Bwn. Emmanuel
Machimo, Afisa Tawala Mahakama ya Wilaya ya Korogwe akipokea cheti kwa kushika
nafasi ya kwanza kwa kada ya Maafisa Tawala/Utumishi Kanda ya Tanga.
Bi.
Elizabeth Noah Mavoa, Mhasibu Msaidizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga,
akipokea cheti kwa kushika nafasi ya pili ya Mhasibu bora Kanda ya Tanga.
Bw. Seif
Mkuya, Dereva bora wa mwaka 2017 akipokea cheti.
Bi. Shehu
Ally Muhsin (Mstaafu) akipokea zawadi.
Hongereni sana Mahakama Tanga kweli mmekuwa vioo vya Mahakama mbali mbali nchini kuanzia kwenye utendaji hata kwenye maswala ya kijamiii bigup Msajili Kabwe na team yako nzima
JibuFuta