Na Angel Meela-Mahakama Kuu kanda ya Moshi
Maafisa TEHAMA wa
Mahakama ya Tanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini wamekutana kwa siku mbili
mjini Morogoro kwa lengo la kuweka mikakati ya kuboresha Utendaji kazi ndani ya
Mahakama.
Katika Mkutano huo wa
mwaka unaoongozwa na Mkurugenzi wa Tehama wa Mahakama ya Tanzania Bw. Kelege
Enock, umewapa nafasi ya kukutana na kuweka mikakati ya pamoja na kujadiliana
masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa kazi zao ikiwemo namna bora ya
kuiwezesaha Mahakama ya Tanzania kufanya shughuli zake kwa kutumia Teknolojia
ya habari na Mawasiliano.
Akifungua Mkutano huo,
Mkurugenzi Msaidizi Bw Machumu Essaba aliwataka Maafisa hao kutumia huo kufahamu
na kufanyia kazi mpango mkakati wa Mahakama na kujadili rasimu ya sera ya ICT
Mahakamani.
Bw. Essaba alitumia
nafasi hiyo kumtambulisha na kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa Tehama ambapo naye
aliwasisitiza Maafisa hao kuelewa majukumu waliyonayo na kupanga mikakati ya
kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Bw. Kelege alisema kuwa
kila mmoja ana maeneo anayoweza kuyafanyia kazi vizuri zaidi kuliko maeneo mengine hivyo kuwataka
washirikiane na kubadilishana uzoefdu walionao ili kuhakikisha wanasonga mbele
katika majukumu yao.
Mkurugenzi
wa Tehama wa Mahakama ya Tanzania Bw. Kelege Enock akizungumza na Maafisa Tehama wa Mahakama ya Tanzania (hawapo) pichani)wakati wa Mkutano wao wa Mwaka unaoendelea mjini Morogoro.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Tehama wa Mahakama ya Tanzania Bw. Machumu Essaba akifungua mkutano wa mwaka wa Maafisa wa Tehama mjini Morogoro.
Maafisa Tehama wakiwa Mkutanoni.
Maafisa Tehama wakiwa Mkutanoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni